30.4 C
Dar es Salaam
Friday, September 24, 2021

Muhimbili yafunga mashine kuhudumia wagonjwa wa figo, corona Amana

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imefunga mashine tatu za kusafisha damu kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana.

Aidha, mbali na mashine hizo zenye thamani ya Sh milioni 210, pia inatarajia kufunga mashine moja ya kusaidia mgonjwa kupumua (ventilator) yenye thamani ya Sh milioni 56. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Hospitali ya Muhimbili leo Jumapili Aprili 26, tayari wagonjwa wanaohitaji huduma ya kusafishwa damu wameanza kuhudumiwa na wafanyakazi wa Muhimbili waliopo Hospitali ya Amana tangu Ijumaa Aprili 24 ambapo dawa na vitendanishi vya kutoa huduma ya kusafisha figo kwa sasa vinagharamiwa na Muhimbili. 

“Sambamba na hilo, Hospitali imefunga mtambo wa kuchuja maji (Portable RO) wenye thamani ya Sh milioni 28 na mtandao wenye miundombinu ya kusafirisha maji ili kuwezesha mashine hizo kufanya kazi ya kusafisha damu uliogharimu Sh milioni 12.

“Kutokana na hilo, Muhimbili itapokea madaktari na wauguzi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Amana kuanzia Aprili 28, mwaka huu ili kujengewa uwezo kwenye Kitengo cha Kusafisha Damu pamoja na vyumba vya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICUs) aina tano tofauti,” amesema Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma wa hospitali hiyo,  Aminiel Aligaesha.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
157,854FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles