26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni ya F.M yamwaga vifaa vya kutakasa mikono Iringa vijijini

RAYMOND MINJA IRINGA

Kampuni ya F.M chini ya  Mkurugenzi wa Kampuni ya. Arifu Abri wamegawa ndoo za kunawia mikono pamoja na vitakasa mikono ikiwa ni kuunga juhudi za Serekali katika kupambana na ugonjwa Wa Corona unaosababishwa  na virusi vya  COVID 19 unaotikisa dunia.

Akizungumza na wananchi Wa kata ya kisinga iliyoko wilaya ya Iringa vijini Mkoani Iringa  Mkurugenzi wa Kampuni Huyo ya . F.M Abri, Alifu Abri wakati wa kugawa msaada wa ndoo maalum za kunawia mikono sabuni za kutakasa mikono, fedha za ununuzi wa barakoa kwa kata ya Hiyo   diwani wa kata hiyo alisema kuwa kampuni hiyo imemeamua kugawa vifaa hivyo hadi Vijijini kwani huko watu walikuwa kama wamesahaulika

Alisema kuwa Vifaa hivyo ambavyo vimetolewa na kampuni hiyo vitasambazwa katika vituo vyote vya afya, kwenye misikiti na kanisani vina thamani ya sh. Milioni 1.2 vitaendana na elimu kwa jamii ili kuweza kuwa na tabia ya kunawa mikono mara kwa mara na kuomba dua kwa MUNGU kuweza kuepukana na maambukizi Zaidi.

“Ndugu zangu Mimi Leo nimekuja nikiwa na vifaa hiii najua munanijua vema na Nina mashamba yangu hapa kata ya kisinga sasa nikasema nije kuwaunga mkono ndugu zangu Mana kama mumesahaulika watu Wa Vijijini lakini nyinyi ni watu muhimu sana ndio Mana tumekuja ndugu zangu ili kupambana na ugonjwa hili linalotikisa dunia

 Abri alisema kuwa huu ni wakati muhimu Wa wazazi na walezi kuwalinda Watoto kutokuambukizwa na virusi hivyo kwani wako katika hatari kubwa zaidi na ndio maana Serekali iliamua kuchukua hatua za kufunga shule zote na vyuo.

Alisema kuwa Watoto wengi wakati huu wamekuwa wakitumia muda wa shule kufunga kucheza michezo mbalimbali hali ambayo inahatarisha kwa kiasi kikubwa usalama wa Maisha yao na kuweza kupata au kuambukizwa virusi vya korona.

Alisema hivi sasa hapa Iringa na Tanzania kwa ujumla kuna watu kadhaa   ambao ni wameambukizwa virusi vya corona hivyo ni muhimu kwa wazazi kuwa makini na Watoto hasa katika mikusanyiko wanayokutana na kuwataka kuwapa elimu ya kubaki ndani kuliko michezo ambayo inasababisha mikusanyiko ambayo serikali imepiga marufuku.

 Alisema zipo changamoto mbali mbali katika ulezi wa Watoto hao,lakini ni vyema wazazi wakaongeza juhudi katika malezi  ili kupata watoto walio bora  hapo baadae na kuondokana na kuambukizwa.

“Mzazi asione tabu kupoteza muda katika kumlelea mtoto wake na kuacha tu akizurura  kwani matunda yake,  atayapata baadae kwani haohao ndio Viongozi wa kesho hivyo muhimu kuwalinda na magonjwa”

Alisema kuwa elimu kubwa inahitajika kwa sasa hasa vijijini kwani ndio sehemu ambayo wengi wameisahau katika kuisaidia kupambana na kusambaa kwa virusi vya Corona.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Kising’a iliyoko jimbo la Ismani, Lita Mlagala akizungumza kwa masikitiko, alisema wakati mwengine watoto wanakufa kutokana na mambo madogo madogo  tu ikiwemo kuwaacha bila uangalizi maalum.

Alisema kuwa katika kata hiyo Watoto wawili wamepoteza Maisha kwa matukio tofauti ikiwemo mmoja kuzama kwenye bwawa na mwingine kupata ajali ya bodaboda hivyo umakini wa wazazi unahitajika sana katika kuwalea na kuwakataza kuzurura.

Alisema kuwa mbaya Zaidi katika kipindi hiki cha janga la Corona ambapo shule zimefungwa Watoto baadhi wamekuwa wakiacha kusoma nyumbani wametumia muda huo kukimbia majumbani na kwenda mijini kufanya kazi mbalimbali.

Mlagala alimshukuru mkurugenzi wa FM Abri , Alifu Abri kwa kwa kuona iko haja ya kutoa msaada huo ambao utasaidia kunusuru Maisha ya wakazi wa Kising’a kwa kutoa msaada na kutaka elimu Zaidi itolewe kwa jamii kuhusu janga la Corona.

“Naamini msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kupambana dhidi ya virusi vya Corona katika kata yet una umekuja wakati mwafaka kabisa hivyo nakushukuru sana Alifu na naomba msaada wa Barakoa kwa vituo vya afya vya kata hii”  alisema.

Aidha alitoa wito kwa makampuni na  taasisi nyingine kuiga mfano wa  mkurugenzi Alifu Abri kwa kutoa misaada   mbali mbali ili kusaidia jamii katika kutatua changamoto  zinazowakabili hasa katika kipindi hiki ambapo dunia anapambana na virusi vya corona

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles