23.2 C
Dar es Salaam
Monday, February 6, 2023

Contact us: [email protected]

MUGABE: NIMEFURAHISHWA NA SERA ZA DONALD TRUMP

HARARE, ZIMBABWE


RAIS wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema anakubaliana na sera ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba ‘Marekani iwe ya Wamarekani’.

Akiuzungumzia kwa mara ya kwanza utawala wa Trump, Mugabe alikiri kushangazwa na ushindi wa kiongozi huyo kutoka Chama cha Republican.

Hata hivyo, amesema hakutaka pia ‘Madam Clinton ashinde’ akimaanisha aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha Democratic aliyeshindwa uchaguzi wa Novemba mwaka jana Hillary Clinton.

“Lakini pia ukija kwa Donald Trump ambapo anazungumzia uzalendo akitaka Marekani iwe ya Wamarekani. Nakubaliana naye katika hilo, Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe,” Mugabe alisema katika taarifa yake iliyochapishwa na gazeti la Serikali la Herald.

Ameongeza kuwa Trump anapaswa kupewa muda wa kudhihirisha uwezo wake.

“Sijui. Mpeni muda. Trump huenda ataangalia upya vikwazo ilivyowekewa Zimbabwe,” Mugabe alisema.

Mahojiano kamili ya Mugabe yalitarajiwa kurushwa rasmi leo jioni ikiwa ni kwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 93 ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles