Mugabe kuzikwa baada ya mwezi mmoja

0
750

HARARE-Zimbabwe

MWILI       wa aliyekuwa Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe umehifadhiwa eneo alilozaliwa,baada ya watu kumuaga katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare.

Viongozi wa Afrika, wamemsifu Mugabe kama mpiganiaji wa uhuru katika mazishi yake Uwanja wa Taifa mjini Harare.

Rais wan chi hiyo, Emmerson Mnagagwa alimtaja Mugabe kama kiongozi aliyekuwa na maono na kusema ‘taifa letu linalia’.

Uwanja ulio na uwezo wa kubeba watu 60,000 ulikuwa na idadi ndogo ya watu.

Uchumi wa taifa hilo upo katika hali mbaya na raia wengi wa Zimbabwe waliamua kususia sherehe hiyo kutokana na ukandamizaji uliotekelezwa na uongozi wa Mugabe.

Kupanda kwa hali ya mfumuko na ukosefu wa ajira ni baadhi ya masuala ambayo yamewafanya raia wa taifa hilo kumlaumu Mugabe.

”Tunafurahia amefariki, kwa nini nihudhurie mazishi yake? sina mafuta”, alisema mkazi mmoja wa Harare akizungumza na AFP.

”Hatutaki kusikia chochote kumuhusu tena. yeye ndio sababu ya matatizo yetu.

Mazishi hayo yanafuatia mgogoro kati ya familia ya Mugabe na Serikali kuhusu mahala atakapozikwa.

Sasa imekubalika  atazikwa makaburi ya mashujaa mjini Harare, familia yake imesema.

Msemaji wa familia na mpwa wake, Leo Mugabe alisema hiyo itafanyika baada ya kipindi cha mwezi mmoja, wakati  kaburi hilo litajengwa.

Awali mipango ya mazishi ilitangazwa ingefanyika jana, lakini ilifutwa.

Mugabe ambaye alikuwa na umri wa miaka 95 alipofariki wiki iliopita alikuwa akitibiwa nchini Singapore.

Viongozi wa Afrika , wa zamani na waliopo sasa waliingia  uwanjani hapo kwa shangwe kubwa pamoja na viongozi waliopigania uhuru wa bara hili.

Sifa za Mugabe kama mpiganiaji uhuru zilitolewa na kila kiongozi ambaye alisimamna kuhutubia akiwemo rais wa Kenya Uhuru kenyatta – huku wakitofautiana na maneno yaliotolewa na mwakilishi wa familia hiyo Walter Chidhakwa aliyesema kwamba ”Mugabe alikuwa na huzuni , huzuni mkubwa’, Ilikuwa safari ngumu na ya kuchukiza”.

Matamashi yake yalionyesha wazi wasiwasi uliopo kati ya serikali iliopo na familia ya Mugabe.

Zaidi ya viongozi 10, wakiwemo wale wa zamani wa mataifa ya Afrika walihudhuria mazishi hayo , wakimsifu Mugabe kama kiongozi wa Afrika aliyeamua kutumikia maisha yake yote kwa raia wa Zimbabwe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here