27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali, taasisi za dini kuendelea kushirikiana

AMINA OMARI Na OSCAR ASSENGA-TANGA

RAIS Dk. John Magufuli, amesema kwamba serikali ina kila sababu ya kuendelea uhusiano mzuri kati yao na madhehabu ya dini nchini kwa sababu kazi wanayoifanya haina mbadala wake kwenye jamii.

Hayo yalisema jana katika hotuba yake ilisomwa na niaba yake na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu  ambapo alimwakilisha katika  Jubilee ya miaka 25 uaskofu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Tanga, Anthony Banzi.

Jubilee hiyo ilikwenda sambamba na ibada iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali Askofu Mstaafu Kadinali Policapy Pengo pamoja na viongozi mbalimbali wakimiwa wa serikali na kisiasa.

Alisema kwamba wanaimani kwa pamoja wanaweza kujenga na kuimarisha kuendelea amani na umoja uliopo hapa nchini wakishirikiana kwa pamoja kuongeza kasi ya watawezesha Watanzania kupata maendeleo.

“Baba Askofu sisi kama serikali tutatimiza wajibu wetu kutengeneza mazingira mazuri kwa madhehebu ya dini kutekeleza wajibu wake kwani uhuru wa kuabudu uliopo nchini unaheshimiwa na kutekelezwa kwa vitendo,” alisema Rais Magufuli katika hotuba yake hiyo

Waziri Ummy alisema kwamba licha ya utofauti za dini, kabila rangi au vyama Rais Dk. Magufuli,  anasema tofauti hizo hatuna budi kuishi nazo na wasiziache zikawa nyufa za uhasama ambao sio zitaligawa taifa bali linaweza kulimonyony’oa hata kanisa.

“Wana Tanga wanayo matumaini makubwa kwa sababu wanathamini na kutambua manufaa makubwa yanayofanya kwenye harakati za kujilete maendeleo kutokana na kazi kubwa mnayoifanya kuwapa maendeleo,” alisema

Awali akitoa salamu za kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Balozi wa Papa hapa nchini, Kadinali Kindondi alisema kuwa mchango waAskofu Banzi ni mkubw kwa kanisa na uhudumu wake wa kazi za kanisa umekuwa ni kichocheo cha maendeleo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles