23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mugabe alikufa kwa saratani

HARARE, ZIMBABWE

SERIKALI nchini Zimbabwe imefichua kuwa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe amefariki kutokana na saratani.

Serikali imeeleza kwamba matibabu ya mionzi ya ‘chemotherapy’ anayepatiwa mgonjwa wa saratani kupunguza sumu mwilini yalisitishwa wakati ilipodhihirika kuwa hayasaidii tena.

Mugabe alifariki mapema mwezi huu nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95.

Anatarajiwa kuzikwa katika kwenye eneo la kitaifa la mashujaa ambalo linajengwa mjini Harare.

Sehemu hiyo ambayo Mugabe atazikwa ni ambapo wapiganiaji uhuru wengi maarufu nchini humo wamezikwa.

Ikiwa ni mara ya kwanza kufichuliwa kwa chanzo cha kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa Zimbabwe, Rais Emmerson Mnangagwa amenukuliwa na vyombo vya habari akiwaambia wafuasi wa chama tawala Zanu- PF mjini New York, ambako amekwenda kuhudhuria mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuwa Mugabe alikuwa na saratani, lakini hakufichua ni saratani ya aina gani.

“Matibabu yalisitishwa, madaktari walikatiza matibabu, chemotherapy, moja, kwasababu ya umri wake na pia kwasababu saratani yake ilikuwa imesambaa na matibabu yalikuwa hayasaidii tena,” Mnangagwa alisema katika matamshi yaliochapishwa kwenye gazeti la serikali la The Herald jana .

Kuondolewa kwake madarakani kulitokana na minong’ono juu ya umri wake ulivyokuwa ukizidi kuongezeka lakini pia afya yake ilivyokuwa ikizidi kuzorota.

Kama ilivyo tabia yake ya kutopenda anasa Mugabe alivaa kawaida na hakutumia kilevi zaidi ya mvinyo kiasi.

Zaidi Mugabe alipenda kufanya mazoezi ya viuongo kila siku.

“Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viungo vya mwili,” alisema Mugabe miaka sita iliyopita.

Alisema huwa anaamka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri.

Siri nyingine ya maisha yake marefu ni kuwa alipenda sana ‘sadza’ – chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe, na ambacho kina virutubisho vingi muhimu.

Vilevile Mugabe alikuwa havuti sigara, ingawa  alikuwa anakunywa mvinyo ‘wine’ kidogo anapokula chakula cha jioni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles