23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mtwara yatenga fedha kukabiliana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele

Na Florence Sanawa, Mtwara

Serikali ya Mkoa wa  Mtwara imewataka viongozi wa Halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha kuwa wanatenga fedha kwaajili ya kuwafikia wananchi na kuwapatia kinga tiba ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Magonjwa hayo ambayo kwa kiasi kikubwa maambukizi yake  bado yapo katika baadhi ya Halmashauri zikiwamo Masasi na Manispaa ya Mtwara Mikindani. 

Akizungumza katika semina ya uraghabishi na uhamasishaji kwa viongozi wa mkoa na Halmashauri iliyoandaliwa na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wazee na Watoto wakishirikiana na shirika lisilo la kiserikali la IMA World Health, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo amesema  magonjwa ya Minyoo ya tumbo, matende na mabusha, trakoma kichocho na usubi kwa kiasi kikubwa yameathiri watu wengi hivyo kupoteza nguvu ya taifa kutokana na magonjwa hayo. 

“Zipo juhudi za Serikali kutokomeza magonjwa haya ambapo kwa mkoa wa Mtwara Wilaya tisa zimeathirika , saba zimeweza kusimamisha matumizi ya dawa kwa ngazi ya jamii,  kiwango cha maambukizi bado kipo juu Manispaa ya Mtwara Mikindani na Masasi na hapo nguvu za ziada zinatakiwa,” amesema.

Naye Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Oscar Kaitaba amesema magonjwa hayo yameongezeka na kufikia 21 ambapo katika mpango huo wanashughulika na magonjwa matano tu ambayo ni Minyoo ya tumbo, mabusha na matende, trakoma, kichocho na usubi. 

“Magonjwa haya yana madhara makubwa yanaongeza umaskini, yanaleta upungufu wa damu, ulemavu, presha ya ini, unaongeza utoro mashuleni na upofu, ndiyo maana tunapanga mikakati ya kuongeza juhudi za kutoa kinga tiba kwa wananchi ili kuwanusuru na athari hizo.

“Ukiangalia kwa mkoa wa Mtwara zipo wilaya zilizokuwa zimeathirika zaidi ambapo Masasi Vijijini bado matende na mabusha lakini kwa Wilaya ya Mtwara bado hali si nzuri kwa magonjwa ya matende na mabusha na trakoma,” amesema Kaitaba.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dk. Sylivia Mamkwe amesema wanapanga mikakati ili kuhakikisha kuwa wilaya ambazo bado maambukizi ni makubwa zinapewa kipaumbele zaidi.

“Mtwara vikope tumefanikiwa tatizo ni tends na mabusha katika wilaya ya Mtwara na Masasi bado kuna maambukizi tunapangaza mikakati ya kupita nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata dawa hata hivyo maeneo ambayo bado maambukizi ni makubwa yana ongezeko la watu wengi na  mwingiliano pia ni mkubwa hata kufikia asilimia 80,”amesema Mamkwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles