24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mtumishi wa Afya kortini kwa tuhuma za kumwomba rushwa mgonjwa

Na Allan Vicent, Igunga

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Igunga mkoani Tabora imemfikisha katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga, Mtumishi wa Idara ya Afya katika Hospitali ya wilaya hiyo, Wallace Kazili (52), kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa mgonjwa.

Akisomewa mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya, Lydia Ulunda, Mwendesha Mashitaka wa TAKUKURU wilayani humo, Mazengo Joseph, amedai mshitakiwa ambaye ni mkazi wa mtaa wa Masanga Kata ya Igunga mjini alitenda makosa hayo kinyume na kifungu cha 15(1)(a) na (2) cha sheria na 11/2007 ya taasisi hiyo.

 Ameieleza Mahakama kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Oktoba 30, 2019 akiwa muuguzi katika hospitali hiyo ambapo aliomba rushwa ya Sh 200,000 kutoka kwa, Kasembe Nangale, ili apatiwe dawa ya kifua kikuu (TB) kwa ajili ya mamake mzazi aliyekuwa amelazwa hospitali hapo.

Joseph amedai kuwa katika tarehe hiyo mshtakiwa alipokea kiasi cha Sh 50,000 kwa njia ya simu kama malipo ya awali ya Sh 200,000 alizoomba na kuongeza kuwa Novemba 1, 2019 alipokea kiasi kingine cha Sh 50,000 kama sehemu ya malipo hayo pia na kufanya jumla kuwa Sh 100,000.

Mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Lydia Ulunda, hivyo kesi hiyo kuahirishwa hadi Aprili 28, mwaka huu, mshtakiwa yuko nje kwa dhamana ya Sh 300,000 ambapo upande wa Jamhuri unategemea kupeleka mashahidi 6 mahakamani hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles