29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Mtoto wa miaka mitatu auawa kwa kushambuliwa na fisi

Na DAMIAN MASYENENE – SHINYANGA

MTOTO wa miaka mitatu Sungwa Kulwa mkazi wa Kijiji cha Dodoma Kata ya Masanga wilayani Kishapu mkoani hapa, amefariki dunia baada ya kushambuliwa na fisi wakati akicheza na watoto wenzake nje ya nyumba yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba jana alisema tukio hilo lilitokea Aprili 30 mwaka huu saa 1:00 jioni katika Kijiji hicho baada ya mnyama huyo kutokea ghafla kutoka vichakani na kumshambulia mtoto huyo.

 Alisema baada ya fisi huyo kuwatokea alimshambulia Kulwa na kumburuza umbali wa mita 100 na kumuachia baada ya kusikia kelele za wananchi waliokuwa wanamfukuza.

Kamanda Debora alisema baada ya tukio hilo kuripotiwa, idara ya wanyamapori Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, ilifika na kutoa elimu ya kujikinga na wanyama hao na kutoa taarifa mapema wanyama wakali wanapotokea.

“Natoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wako katika mazingira salama muda wote wasiachwe peke yao, wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari hasa kipindi hiki ambacho fisi wamekuwa wakionekana maeneo mbalimbali ya mkoa wetu,” alisema Kamanda Debora.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,609FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles