25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto aliyeuzwa Sh 30,000, akabidhiwa wazazi wake akiwa na miezi tisa

NA AMON MTEGA

SONGEA

IKIWA ni takribani miezi tisa tangu Septemba 26 mtoto Shazira Yahaya (miezi 9) kuibiwa akiwa na siku saba na kuuzwa kwa Sh 30,000, jana alikabidhiwa kwa wazazi wake.

Wakati mtoto huyo akikabidhiwa kwa wazazi wake,askari polisi F.2229D/CPL Victor aliyefanikisha kupatikana kwake, yeye alikabidhiwa Sh 300,000 kutokana na kazi aliyoifanya.

Shazira alikabidhiwa kwa mama yake mzazi Amina Abdallah (17) jana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.

Makabidhiano hayo yalifanyika baada ya watuhumiwa wa tukio hilo Abrahamu Kilewa (20) mkazi wa Kijiji cha Mahanje Halmashauri ya Madaba mkoani humo na Anosiata Luambano (36) mkazi wa Kijiji cha Mambakokirie Wilaya ya Moshi vijijini kuhukumiwa kifugo cha miaka miwili jela kila mmoja. 

Mndeme akikabidhi mtoto huyo kwenye ofisi za Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma  ACP, Simon Maigwa, alilipongeza jeshi la polisi mkoani humo kwa kazi waliyofanya.

 Alisema kufuatia kazi iliyofanywa na Askari Victor ya kujituma, ofisi yake imeamua kumpatia zawadi ya Sh 300,000 ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake.

 Aliwataka wanawake wenye shida ya watoto wafuate taratibu za kupata watoto kwenye vituo vya kulelea watoto na siyo kuiba kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa, alisema mtoto Shazira aliibiwa Septemba 26 mwaka jana saa 3:00 usiku katika Kijiji cha Likalangiro Wilaya ya Songea.

Alisema mtoto huyo aliibiwa na Abrahamu Kilewa kisha kumuuza kwa Anosiata Luambano kwa Sh ,30,000 ambapo mnunuzi huyo aliondoka naye na kwenda naye Marangu Moshi anakoishi mpaka Februari alipokamatwa.

“Mtoto huyu aliibiwa akiwa na siku saba na alipatikana akiwa na miezi mitano na sasa ana miezi tisa. Madaktari  wamethibitisha kuwa ni mwenye afya njema, ” alisema Kamanda Maigwa.

Mama wa mtoto huyo Amina Abdalah, aliishukuru Serikali ya mkoa na polisi kwa kufanikisha kumpata mtoto huyo.

 Pia Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Songea, Victor Nyenja, alisema mtoto Shazira baada ya kupatatikana alikuwa akitunzwa na ustawi wa jamii wakati kesi za watuhumiwa zilipokuwa zikiendelea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles