31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Mtalii afa maji akimchumbia mpenzi wake ndani ya bahari

MWANDISHI WETU-PEMBA

MWILI wa raia wa Marekani, Steven Weber anayedaiwa kufa maji  akiwa anamchumbia mpenzi wake, Kenesha Antoine kisiwani pemba, umekabidhiwa kwa ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Weber ambaye alifika visiwani humo kwa ajili ya mapumzikoi, anadaiwa kufa maji wakati akiogelea kutoka chini ya bahari usawa wa chumba hicho alikokwenda kumuonyesha mpenzi wake ujumbe wa mapenzi aliomuandikia pamoja na pete kupitia kioo ambacho mtu aliyeko chumbani anaweza kushuhudia kila kitu kinachoendelea chini ya maji.

Weber na Kenesha kutoka eneo la Baton Rounge mjini Luoisiana Marekani, walipanga chumba hicho kilichozungukwa na vioo kilichopo chini ya maji katika hoteli moja kisiwani Pemba.

Ujumbe  ulioandikwa kwanye karatasi hiyo ulisomeka “Siwezi kuzuia pumzi zangu kwa muda mrefu ili kukwambia kila kitu ninachokipenda kwako, lakini kila kitu ninachokipanda kwako nakupendea zaidi kila siku,”ulisomeka ujumbe huo.

Baadaye Weber aliibadilisha karatasi hiyo ili kuonyesha maneno aliyokuwa ameandika upande mwengine yaliosema: “Je tafadhali unaweza kuwa mke wangu? Utafunga ndoa nami?

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Marekani (CNN), baadaye alitoa pete ya uchumba kutoka katika mfuko wake kabla ya kuogelea na kuondoka eneo hilo.

Antoine naye alichapisha picha za kisa hicho katika facebook ambapo anaonekana akifurahia pamoja na tamko lake: Ndio! Ndio! Ndio!.

Lakini mrembo huyo, baadaye alichapisha habari mbaya kwamba mpenzi wake amefariki dunia.

Antoine alisema hakurudi akiwa mzima baada ya kuogelea baharini.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ilisema mtalii mmoja wa Marekani amefariki nchini Tanzania, lakini hakuna maelezo zaidi yaliyoripotiwa.

Antoine aliandika: “Hakuna maneno yatakayotoa heshima kwa mpenzi wangu Steven Weber Jr.

“Hukutokezea tena kutoka kina hicho cha bahari, basi hukuweza kusikia nikikubali mara milioni kwamba ndio nitafunga ndoa nawe!

“Hatukuweza kukumbatiana na kusherehekea mwanzo wa maisha yetu yaliosalia, baada ya siku bora zaidi katika maisha yetu kuwa mbaya zaidi”.

“Nitajaribu kujifariji kwa kuwa tulifurahia siku zetu za hivi karibuni na kwamba sote tulikuwa tumejawa na furaha wakati wetu wa mwisho”.

Akizungumza na waandishi wa Habari viziwani humo jana, Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Abdallah Mohamed alisema taarifa kutoka kituo cha Konde, Pemba zinaeleza mtalii huyo alifariki akiwa anaogelea.

Alisema mwili wa Weber, umechukuliwa na ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa ajili ya uchunguzi zaidi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles