22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

MSICHANA AOKOLEWA MSITUNI, ANA TABIA ZA TUMBILI

Na MWANDISHI WETU


POLISI kaskazini mwa India wanachambua orodha walizo nazo za watoto waliopotea wakijaribu kumtambua msichana mmoja ambaye anadaiwa amekuwa akiishi na nyani.

Msichana huyo mwenye umri wa kati ya miaka minane na 10 alipatikana wiki chache zilizopita katika msitu eneo la Uttar Pradesh.

Madaktari wanasema msichana huyo hawezi kujieleza na anaonyesha mienendo na tabia kama za nyani.

Ofisa wa polisi, Suresh Yadav alisema walipoenda kumuokoa msichana huyo, walimkuta akicheza na kundi la nyani huku akionyesha tabia kama zao.

Aligunduliwa na wanakijiji katika mbuga ya wanyamapori iliyoko katika mpaka wa India na Nepal.

Yadav alisema walipofika kumchukua walivamiwa na kundi la nyani.

Madaktari wanasema alikuwa anaugua utapiamlo, pia kucha na nywele zake zilikuwa ndefu kupita kiasi.

“Alikuwa na vidonda mwilini, pia alikuwa hawezi kuwasiliana kwa njia yoyote ile. Alitembea kwa kutumia mikono na miguu yote,” alisema ofisa huyo.

Alisema kuwa hali yake inaendelea kuwa bora na mwishowe atapelekwa kwenye shirika la watoto watakaosaidiana na madaktari bingwa kumfunza mienendo ya binadamu.

Mganga Mkuu wa hospitali aliyolazwa, Dk. Singh alisema BBC Hindi kuwa mtoto huyo atahamishwa na kupelekwa katika chuo cha matibabu cha Lucknow mara tu madaktari watakaporidhika na hali yake ya afya.

Huko atapata matibabu na usaidizi zaidi.

Hakimu wa Wilaya, Ajaydeep Singh alimtembelea msichana huyo hospitalini na amempa jina la Forest Durga linaloashiria shujaa wa Kihindi.

Wengi nchini India wanamfananisha msichana huyo na Mowgli, msichana aliyelelewa na mbwa mwitu katika kitabu cha Rudyard Kipling cha Jungle Book.

Hata hivyo mpaka sasa haijajulikana ni kwa muda gani msichana huyo aliishi msituni.

Imeandaliwa kwa msaada wa BBC

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,215FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles