23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

MSIBA WA TAIFA

Na RAMADHAN LIBENANGA

– MOROGORO

NI majonzi. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta kupinduka mjini Morogoro na kusababisha watu zaidi ya 60 kufariki dunia na wengine 70 kujeruhiwa walipokuwa wakichota mafuta.

Hadi tunakwenda mtamboni jana, mmoja wa Ofisa wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alisema mpaka jioni vifo vilikuwa 64 na majeruhi 70.

Kwa mujibu wa baadhi ya mashuhuda, ajali hiyo ilitokea jana asubuhi majira ya saa mbili baada ya dereva wa lori kumkwepa mwendesha pikipiki na baadaye kushindwa kulimudu gari lake na kupinduka.

Walisema baada ya gari hilo kupinduka, dereva alijaribu kuonya wananchi kutosogea karibu kwa sababu lilikuwa limebeba petroli na lingeweza kuwaka moto wakati wowote.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, baadhi ya vijana wengi wao wakiwa waendesha bodaboda na wapigadebe Kituo cha Mabasi Msamvu, hawakusikia onyo hilo na wakaendelea kuchota mafuta.

Walisema vijana hao na baadhi ya mama lishe waliokuwa karibu na eneo hilo, walichota mafuta hayo kwa takribani nusu saa kabla ya wenzao kwenda eneo la betri ya gari hilo wakijaribu kuzitoa ndipo moto ukawaka.

HOSPITALI

Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Ritha Lyamuya, alisema kwa asubuhi alipokea miili ya watu 62 na majeruhi 70.

“Mpaka sasa tayari tumeshapokea miili ya watu 62 katika ajali hiyo ya moto na majeruhi 70 wamelazwa katika hospitali yetu,” alisema Dk. Lyamuya.

POLISI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mtafungwa, alithibitisha watu 62 kufariki dunia katika ajali hiyo na majeruhi wakiwa ni 70.

Alisema lori hilo …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles