22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 29, 2022

MSHTUKO POLISI WATATU KUJIUA NDANI YA SAA 24

ANDREW MSECHU Na PATRICIA KILEMETA-DAR ES SALAAM          |    


MATUKIO ya kujiua kwa askari polisi watatu ndani ya saa 24, yameibua mshtuko kwa jamii kuhusu sababu zinazowasukuma kuchukua hatua hiyo.

Askari hao wamejiua kwa kujipiga risasi katika matukio yaliyotokea mikoa mitatu tofauti ya Mara, Tabora na Morogoro, huku kila mmoja akitoa sababu za kuondoa uhai wake.

Katika tukio la kwanza, polisi mwenye cheo cha konstebo, G 3777 Nelson William, alijiua kwa kujipiga risasi kutokana na wivu wa mapenzi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 8 mchana akiwa eneo la kambi za polisi alikokuwa anaishi.

Alisema kabla ya kujipiga risasi, aliacha ujumbe kuwa ameamua kujiua kutokana na wivu wa mapenzi, kwa madai amekuwa hana uhusiano mzuri na mwanamke ambaye alikuwa ni mpenzi wake.

“Askari huyu kabla ya kuchukua uamuzi huo, aliingia kwenye malumbano na mpenzi wake. Baada ya kwenda kwenye chumba cha mpenzi wake, aliamua kuharibu mali alizonunua.

“Baada ya tukio hilo la kuharibiwa mali, mwanamke huyo ambaye ni mpenzi wa askari huyo, aliamua ….

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,204FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles