21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

RC MTAKA: WANANCHI CHANGAMKIENI UWEPO WA MWIBA HOLDING

Na Elia Mbonea

Wananchi  wa Mkoa wa Simiyu, Arusha, Mara, Shinyanga na Mwanza wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotokana na uwekezaji unaofanywa na Kampuni ya Kitalii ya Mwiba Holding Ltd katika Pori la Akiba Maswa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akiwa kwenye ziara ya Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Simiyu na Kamati ya Siasa ya CCM mkoa na wilaya ya Meatu.

Akiwa kwenye eneo la uwekezaji wa Mwiba Holding RC Mtaka alisema uwekezaji uliofanywa na kampuni hiyo umekuwa na faida zaidi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

“Mwiba Holding wamewekeza eneo la Hifadhi ya Jamii ya wanyamapori(WMA) ya Makao na eneo la Ranchi Kijiji cha Makao, wanatoa Sh milioni 610 kwa vijiji saba vinavyozunguka hifadhi kila mwaka, wanachangia misaada na kutoa ajira,”

“Kampuni hiyo, pia inachangia shughuli za maendeleo na hivi karibuni, imetoa saruji mifugo 3000, mabati 1000 na zaidi ya Sh milioni 115 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa elimu wa mkoa wa Simiyu,” alisema Mtaka.

Kwa upande wake mmoja wa Wakurugenzi wa Taasisi ya Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed, alisema kampuni za Mwiba Holding, Tanzania Game Trackers Safaris(TGTS) na Wingert  Safaris zimewekeza zaidi ya Sh Bilioni 670 ambapo mwaka huu pia wanatarajia kuongeza Sh bilioni 227.

“Tunatarajia kuongeza uwekezaji ila tunachoomba mazingira bora ya uwekezaji kuondolewa migogoro katika maeneo yetu, ikiwapo uvamizi wa mifugo na kama kuna mapungufu tuelezwe,”alisema Mohamed.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji Taifa, Jackson Yuma alitaka uongozi wa serikali kutokubali eneo la makao liharibiwe kwa kuruhusu mifugo kuingia ndani ya hifadhi hiyo.

Yuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM mkoa wa Simiyu, alitaka serikali kwa kushirikiana na wawekezaji kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi yanatunzwa kwa gharama zote kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Aidha, Mkuu wa wilaya ya Meatu, Dk. Joseph Chilongani alisema wilaya hiyo imeanza kunufaika na wawekezaji wa sekta ya utalii hivyo aliomba migogoro isiyo ya lazima itatuliwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles