31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mshikemshike Ligi Kuu England leo

LONDON, ENGLAND

NYASI za viwanja saba vya Ligi Kuu nchini England zinatarajia kuwa na wakati mgumu kutokana na michuano hiyo kuendelea leo.

Wagonga nyundo wa jiji la London, West ham ambao wanashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi, leo hii watakuwa kwenye uwanja wao wa Boleyn Ground na kuwakaribisha washika bunduki, Arsenal ambao wapo nafasi ya tatu katika msimamo.

West Ham wanahitaji kushinda ili waweze kupanda nafasi moja huku wakiwaombea mabaya Man United katika mchezo wao dhidi ya Tottenham ambao utapigwa kesho huku wakiwa nafasi ya tano na kuwaacha West Ham pointi mbili.

Hata hivyo, Arsenal wanahitaji ushindi japokuwa bado watakuwa wanasalia katika nafasi hiyo ya tatu hata kama wakapoteza ama kushinda.

Aston Villa ambao wanaburuza mkia watakua nyumbani Villa Park kuwakabili Bournemouth ambao wanashika nafasi ya 13, bado Aston Villa wana wakati mgumu katika mchezo huu na tayari wapo kwenye taa ya kushuka daraja msimu huu.

Man City watashuka katika uwanja wao wa Etihad kusaka pointi tatu kwa kucheza na West Bromwich Albion, huku Swansea wakikipiga na Chelsea mchezo utakaochezwa katika dimba la Libert. Michezo mingine ambayo itapigwa leo ni pamoja na Crystal Pale na Norwich, Southampton dhidi ya Newcastle, huku Watford ikipambana na Everton.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles