Baba wa James amkataa Zidane kuwa kocha

0
1083

135062MADRID, HISPANIA

BABA wa kiungo wa Real Madrid, James Rodriguez, Wilson Rodriguez, amesema kwamba uteuzi wa Zinedine Zidane kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kunamwathiri mtoto wake.

Wilson amedai mbali na mwanawe kuwa majeruhi, lakini Zidane hampi nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo kiwango chake kinashuka.

James ambaye ni raia wa nchini Colombia, alijiunga na klabu hiyo ikiwa chini ya kocha Carlo Ancelotti mwaka 2014 na kufurahia msimu wa kwanza, lakini baada ya hapo bado hajawa sawa sawa na Zidane anashindwa kutoa msaada wa kutosha kwa mchezaji huyo.

“Najua soka ndivyo lilivyo, kuwa majeruhi ni jambo la kawaida kwa mchezaji na kumfanya mchezaji kushindwa kulinda kiwango chake.

“Uwepo wa Ancelotti na Zidane ni vitu viwili tofauti, wakati wa Ancelotti mwanangu alikuwa anapata nafasi ya kucheza, lakini ujio wa Zidane mambo yamebadilika,” alisema Wilson.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here