27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Msama Promotion waja na Tamasha la Shukurani Oktoba 3, Upendo Nkone…

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Wasanii wa Injili nchini wanatarajia kufanya Tamasha kubwa la shukurani katika Uwanja wa Uhuru litakalofanyika Oktoba 3, 2021 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama(kulia) akiimba pamoja na Mwimbaji Upendo Nkone, wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari. Picha na Beatrice Kaiza.

Akizungumza Dar es Salaam Agosti 21, Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, amesema kuwa tamasha hilo linatarajia kuhusisha waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili nchini.

Aidha, Msama amesema hiyo itakuwa ni sehemu ya ujio wa matamasha yanayoandaliwa na kampuni yake baada ya kuwa kimya kwa takribani miaka sita.

“Mashabiki wakae mkao wa kula kwani tumekaa kimya ndani ya miaka sita. Hivyo katika tamasha hili la shukurani tutakuwa na waimbaji wakubwa wa injili wanaofanya vizuri hapa nchini wakiwamo Upendo Nkone, hivyo nniwaombe wakazi wa Dar es Salaam kukaa mkao wa kula kwani awamu hii itakuwa balaa.

“Mwenyezi Mungu ametupatia kibali cha kumsifu, hivyo tumerudi na niwaombe Watanzania wakae tayari kwa ajili ya kupokea matamasha yetu kama ilivyokuwa hawapo awali,” amesema Msama.

Upande wake, Mwimbaji, Upendo Nkone amewataka Watanzania kujiandaa na tamasha hilo na kwamba wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya kutoa huduma ambayo Watanzania wameikosa kwa kipindi kirefu kupitia matamasha ya Msama Promotion.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles