23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mpinzani wa Urusi aliyepewa sumu aanza kutembea

BERLIN, UJERUMANI

MWANASIASA wa upinzani wa Urusi, Alexei Navalny ameonekana akishuka ngazi katika picha aliyosambaza kupitia mtandao wa instagram jana, ikiwa ni siku tano baada ya hospitali inayompatia matibabu ya mjini Berlin kusema ameondolewa mashine ya kumsaidia kupumua na anaweza kumudu pia kupumua mwenyewe. 

Navalny, ambae ni mpinzani Rais Putin wa Urusi, aliugua mwezi uliopita jimboni Siberia na akasafirishwa kupelekwa Berlin. Ujerumani imesema vipimo vya kimaabara katika mataifa matatu vimebaini kuwa aliwekewa sumu aina ya Novichok, ambayo inauwa mishipa ya fahamu, na mataifa ya Magharibi yameshinikiza kupata maelezo kutoka Urusi. 

Katika ukurasa wa Instagram Navalny ameandika ” Acha nieleze namna ninavyoendelea kupata unafuu. Tayari imeshaonenekana njia kuwa nyeupe sana,” ingawa bado ndefu.”

Navalny alisafirishwa Ujerumani baada ya kuanza kuugua akiwa ndani ya ndege huko Siberia mwezi uliopita na hadi sasa bado amepoteza fahamu.

Timu yake inasema alitiliwa simu kwa maagizo ya Rais Vladimir Putin. Hata hivyo Urusi imekanusha madai hayo.

Msemaji wa Urusi aliitaka Ujerumani kuishirikisha taarifa zake zote huku Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Maria Zakharova akilalamika kwamba madai ya Novichok hayakuambatinishwa na ushahidi wowote. “Ukweli uko wapi, ni mchakato gani uliotumika, yaani hata mtoe taarifa?” alisema.

Sumu inayoathiri neva ya Novichok ilitumiwa kwa aliyekuwa jasusi wa Urusi Sergei Skripal na binti yake wakiwa Uingereza mwaka 2018. Ingawa wao walinusurika, mwanamke mwingireza alifariki baadae akiwa hospitalini. 

Uingereza ilishutumu jeshi la Uingereza kwa kutekeleza shambulio hilo.

Jina Novichok maana yake ni “mgeni” kwa lugha ya Kirusi.

Ni jina linalotumiwa kurejelea kemikali za sumu ambazo hushambulia mfumo wa neva mwilini.

Kemikali hizo ziliundwa na Muungano wa Usovieti miaka ya 1970 na 1980.

Zilifahamika kama silaha za kemikali za kizazi cha nne na zilistawishwa chini ya mpango wa silaha za Muungano wa Usovieti uliofahamika kama “Foliant”.

Mwaka 1999, maofisa wa ulinzi kutoka Marekani walisafiri hadi Uzbekistan kusaidia kuvunja na kusafisha moja ya eneo kubwa zaidi lililotumiwa kufanyia majaribio silaha za kemikali na Muungano wa Usovieti.

Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa ngazi za juu ambaye alitorokea Marekani, maofisa wa Usovieti walitumia kiwanda kilichokuwa eneo hilo kuunda na kufanyia majaribio sampuli za kemikali ya Novichok. 

Kemikali hii iliundwa mahsusi kutoweza kugunduliwa na wakaguzi wa silaha na sumu katika mataifa mengine.

Madaktari walimtibu Alexei Navalny kwa siku tatu pekee kabla ya kuhamishwa hadi hospitali ya Charité mjini Berlin nchini Ujerumani.

Sumu hiyo pia inaelezwa kuwa ni yenye nguvu kuliko sumu nyingine

Moja ya kemikali hizi zinazofahamika kama Novichok – A-230 – inadaiwa kuwa na nguvu mara 5-8 zaidi ya sumu nyingine hatari kwa jina VX.

“Hii ni sumu hatari na changamano kushinda sumu aina ya sarin au VX na pia huwa vigumu zaidi kuitambua,” anasema Prof Gary Stephens, mtaalamu wa kemikali katika Chuo Kikuu cha Reading.

Sumu ya VX ndiyo iliyotumiwa kumuua ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un mwaka jana, kwa mujibu wa Marekani.

Aina mbalimbali za kemikali hii ya A-230 zimekuwa zikitengenezwa, na aina moja inadaiwa kuidhinishwa na jeshi la Urusi itumike kama silaha ya kemikali.

Ingawa baadhi ya aina za sumu hii ya Novichok huwa majimaji, kuna aina nyingine ambazo ni yabisi (ngumu au isiyokuwa majimaji).

Ni kemikali ambayo pia inaweza kugeuzwa kuwa poda laini.

Baadhi ya sumu hizi pia hudaiwa kutumiwa kama silaha za ngazi mbili.

Hii ina maana kwamba sumu hii huhifadhiwa mara nyingi kama kemikali aina mbili ambazo zikiwa kando kando si hatari.

Zinapochanganywa, huingiliana na kutengeneza sumu.

Hii huifanya rahisi sana kwa viungo vya kemikali hii kusafirishwa kwani huwa sumu tu zikichanganywa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles