23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 8, 2024

Contact us: [email protected]

Moto wa Asa, Wizkid usipime…

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

SIKU chache baada ya kuachia ngoma mbili kwa mpigo za Mayana na Ocean, staa mrembo kutoka nchini Nigeria, Asa amezindua rasmi albamu yake yenye ngoma kumi ndani yake, akiwashirikisha wakali kibao akiwemo staa mkubwa wa muziki nchini hu Wizkid.

Katika albamu hiyo aliyoipa jina la V (Five), Asa pia amewashirikisha wakali wengine kibao, akiwemo Amaarae na The Cavemen ambapo imesheheni nyimbo zenye mahadhi tofauti, kuanzia Pop, Afrobeat na R&B.

Akiizungumzia albamu hiyo, Asa amenukuliwa akisema mchanganyiko wa nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo, ni uthibitisho kwamba muziki wake umekuwa ukibadilikabadilika na kuzidi kupanga ngazi kila kukicha kwa lengo la kukata kiu ya mashabiki wake.

Mwanadada huyo anaelezea kwamba safari hii, nyimbo zote amezitunga akiwa jijini Lagos ambapo kuzuka kwa ugonjwa wa Corona, kulifanya ratiba zake zote za ziara za kimuziki kusitishwa na hivyo kumpa muda wa kutosha wa kutulia na kuandaa kazi yenye ubora wa hali wa juu.

“Nilikuwa nyumbani nikifikiria nini cha kufanya kama watu wengine wote walivyokuwa wakifanya kipindi cha Corona. Kwa hiyo nikapata nafasi ya kukutana na marafiki zangu na kila mmoja kuonesha ubunifu wake. Nilikutana na Prodyuza Priime na hakika ni mtu mzuri sana kwenye suala la production na hapo ndipo albamu yangu ilipozaliwa,” amesema Asa.

Anaongeza kuwa mwanzo hakuwa anajua kwamba tayari safari ya kutengeneza albamu imeanza, alidhani anaandaa nyimbo moja moja lakini uwezo aliokuwa akiuonesha kila anapoingia studio, na umahiri wa prodyuza Priime, ulimfanya ajikute tayari amekamilisha albamu iliyosheheni ngoma kali tupu.

Ngoma zilizopo kwenye albamu hiyo ni hizi; Mayana, Ocean, IDG aliomshirikisha Wizkid na Nike.

Nyingine ni Show Me Off, Morning Man, Good Times aliofanya kolabo na The Cavemen, Believer, All I Ever Wanted hapa amesimama na  Amaarae; kisha Love Me Or Give Me Red Wine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles