29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

MOI WAFANYA UPASUAJI UTI WA KIBIYONGO

Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk. Othuman Kiloloma
Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk. Othuman Kiloloma

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) imefanya   upasuaji mwingine wa kunyoosha uti wa mgongo.

Akizungumza na MTANZANIA   jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma MOI, Almas Jumaa, alisema upasuaji huo ulifanyika wiki iliyopita.

Alisema madaktari bingwa wa MOI walifanya upasuaji huo kwa kushirikiana na wenzao kutoka Hospitali ya COEDN ya   Marekani.

“Wataalamu hao wamemfanyia upasuaji huo mkubwa wiki iliyopita, Nadhifa Seleman (13), ambaye alikuwa na tatizo la kupinda uti wa mgongo (kibiyongo),” alisema.

Alisema hiyo ni mara ya pili kwa madaktari wa hospitali hiyo kufanikisha upasuaji huo ambao  ulikuwa haufanyiki  nchini.

“Upasuaji wa kwanza ulifanyika Oktoba 5 mwaka jana… tulishirikiana na hawa hawa madaktari.

“Kwa hiyo tunaendelea kujiimarisha kusudi kila anayehitaji upasuaji wa aina hii aweze kupata huduma   nchini,” alisema.

Hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi wa MOI, Dk. Othuman Kiloloma alisema   wagonjwa waliokuwa wakihitaji kufanyiwa upasuaji wa aina hiyo walikuwa wakipewa rufaa kwenda India.

“Kwa mwaka walikuwa wakipelekwa watoto kati ya 15 hadi 20 na kila mtoto mmoja alikuwa akilipiwa na serikali kati ya Dola 60,000 hadi dola 80,000 (Sh milioni 125 hadi Sh milioni 130),” alisema.

Alisema   kufanyika kwa upasuaji huo nchini kutasaidia kuokoa fedha hizo na   wataweza kusaidiwa wagonjwa wengi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles