25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Mohamed Salah aliza shabiki Napoli

LIVERPOOL, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa timuya Liverpool, Mohamed Salah, juzi alimliza shabiki wa timu ya Napoli kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kupachika bao kwenye Uwanja wa Anfield.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa hatua ya makundi, ulionekana kuwa na ushindani wa hali ya juu,lakini Salah aliweza kuwapeleka Liverpool hatua ya 16 bora baada ya bao lake katika dakika ya 34 dhidi ya Napoli.

Katika mchezo huo,Liverpool ilikuwa inahitaji ushindi ili kuweza kusonga mbele, wakati huo Napoli ikihitaji sare au ushindi, lakini bao la Salah liliweza kuzima ndoto za timu hiyo kusonga hatua inayofuata.

Baada ya bao hilo, dakika ya 38 shabiki wa Napoli alimulikwa na kamera huku ikimwonesha akiwa analia kutokana na kuumizwa na bao hilo, huku mashabiki wengine wakiwa hawaamini kilichotokea.

Napoli walikuwa na nafasi kubwa ya kusonga mbele kwa kuwa waliweza kuumiliki mchezo na kutengeneza nafasi nyingi, lakini walishindwa kuzitumia ikiwamo nafasi zile katika dakikaza lala salama.

Mbali na Liverpool kufuzu hatua ya 16 bora, kwa upande mwingine klabu ya Tottenham nayo imefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Barcelona.

Tottenham walikuwa kundi B ambalo linaongozwa na Barcelona, lakini walikuwa na ushindani wa kuwania kufuzu dhidi ya Inter Milan, huku Barcelona wakiwa wa kwanza kufuzu,ila Inter Milan walishindwa kutamba mbele ya PSV ambapo mchezo huo ulimalizikakwa sare ya 1-1 na kuwafanya Inter Milan washindwe kusonga mbele.

Kundi A, Atletico Madrid na Borrusia Dortmund wamefanikiwa kufuzu, wakati huo kundi C ni PSG na Liverpool, huku FC Porto na Schalke 04 wakifuzu kundi D.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles