30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Simba yatua Kitwe kibabe

HUSSEIN OMAR-DAR ES SALAAM

WAWAKILISHI waTanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika,Simba, wamewasili jana Zambia kwa kishindo, tayari kusaka ushindi katika mchezo wa raundi ya kwanza dhidi yaNkana FC.

Simba iliyosafiri na Shirika la Ndegela Ethiopia ikiwa na wachezaji 30, ilipokewa na Watanzania wanaoishi nchini Zambia jana mchana.

Timu hiyo itavaana na Nkana FC Jumamosi katika Uwanja wa Nkana mjini Kitwe na baadaye kurudiana Desemba 23,mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi ambao mara ya mwisho kucheza michuano hiyo ni mwaka 2013, wataingia kwenye mchezo huo baada ya kuwatoa Mbabane Swallows kwa ushindi wa mabao 8-1, baada ya kushinda mabao 4-1katika mchezo wa kwanza mjini Dar es Salaam, kabla ya kuwachapa wapinzani waohao wakiwa kwao mabao 4-0.

Wapinzani wao Nkana FC iliwatoa UD Songo ya Msumbiji kwa mabao 3-1, ikishinda mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza na baadaye bao 1-0 katika mchezo uliochezwa mjini Kitwe.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Meneja wa Simba, Abasi Ally, alisema kikosi hicho kimewasili salama na leo jionikitafanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo ambao umevuta hisia za mashabiki wengi nchini Zambia.

“Tunashukuru tumepata sapoti kubwasana kutoka kwa Watanzania ambao wanaishi hapa na wametuahidi siku ya mchezo watakuja kwa wingi kutupa sapoti,” alisema Ally.

Alisema kubwa lililopo kwa sasa kwenye kikosi hicho ni kupata matokeo katika mchezo huo wa marudiano ili waweze kusonga mbele hatua inayofuata.

“Ni mechi ngumu, tunafanya mikakati ya ndani na nje ya uwanja kuhakikisha hatupotezi mchezo huo na tunaibuka na ushindi mnono ili kusonga mbele,” alisema Ally.

Alisema katika kuzingatia hilo kumekuwepo na ulinzi mkali katika hoteli waliyofikia kwa ajili ya kuweka mambo sawa wakihofia kufanyiwa hujuma na wapinzani wao hao.

Ally alisema wamepata mapokezi makubwa kutoka kwa Watanzania  ambao wanaishi nchini humo na kuwaahidi kutowaangusha siku hiyo ya mchezo kwani wamejipanga vyema kila idara.

 “Tunawashakuru kwa kweli mashabiki wote waliojitokeza kuja kutupokea, tuna deni la dakika tisini nyingine ambazo benchi la ufundi likiongozwa na Patrick Aussems, litafanya vizuri na kupata matokeo mazuri zaidi ya mechi ya mwanzo.

Katika hatua nyingine mchezo huo umekuwa gumzo nchini Zambia kutokana na Watanzania wanaoishi nchini humo kuwatambia wenzao kuwa Simba ni timu kubwa Afrika.

Mtanzania mmoja anayeishi nchini humo,Daudi David, aliliambia MTANZANIA kuwa mchezo huo umekuwa gumzo kila kona kutokana na kuzungumziwa kwake ukilinganisha na michezo mingine iliyowahi kuchezwa.

Alisema wao kama wapenda soka wamejipanga kwenda kwa wingi uwanjani Jumamosi kwa ajili ya kuishangilia Simbaambayo wanaiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa.

“Huu mchezo ni mkubwa sana kila kukicha masokoni, madukani, mitaani watu wanauzungumzia kwa kweli na sisi tumejipanga kuwapa sapoti Simba,” alisema.

 “Tunawaomba Watanzania tunahitaji dua zao na sala ili kupata matokeo mazuri na kusonga mbele katika raundi hii ya kwanza, hivyo waendelee kutupa sapoti,” alisema.

Simba itaingia uwanjani ikijivunia kuwa na safu hatari ya ushambuliaji inayoongozwa na Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na John Bocco pamoja na kiungo mshambuliaji, Cletous Chama.

Nkana wakitamba kuwa na washambuliaji kama Walter Bwalya na Ronald Kampamba,  huku wakimkosa  kinara wao wa mabao, Idris Mbombo,aliyejiunga na Al Ahly ya Sudan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles