25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mo Dewj atua Fifa, ateta na Infantino

Winfrida Mtoi – Dar es Salaam

MWEKEZAJI na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji ‘Mo’, amekutana na Rais Shirikisho la Soka la Kimataifa(FIFA), Gianni Infantino na kufanya naye mazungumzo.

Mo alitembelea makao makuu ya shirikisho hilo yaliyopo Zurich, Uswisi jana, baada ya mazungumzo alimkabidhi Infantino jezi ya Simba.

Katika picha ambazo Mo anaonekana akiwa anamkabidhi rais huyo jezi, aliandika maneno yanayosema: “Nimefurahishwa na dira na shauku ya kuendeleza soka la ushindani na kuvutia Afrika.

“Leo (jana) nimekutana na Gianni Infantino, Rais wa FIFA katika makao makuu yao, kwa kweli nimefurahishwa sana, kwa dira na shauku ya kuendeleza mpira wa ushindani na wa kuvutia Afrika.

“Nia yao ni kuboresha maendeleo ya mpira, najua, chini ya uongozi wa Infantino mpira wa miguu kwenye bara letu utaenda ‘next level’ (hatua nyingine), aliandika Mo.

Kabla ya kuweka picha ya Infantino, wiki iliyopita Mo alitupia picha akiwa na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles