23.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

MNEC Jumaa anza ziara Kibaha Vijijini, asifu kazi kubwa ya Rais Samia

ANa Gustafu Haule, Pwani

MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) kupitia Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamou Jumaa, amefanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa katika Wilaya ya Kibaha Vijijini kwa kipindi cha miaka miwili huku akisifu jitihada za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

Jumaa amefanya ziara hiyo leo  Juni 8, katika kata mbalimbali zilizopo Kibaha Vijijini huku akiongozana na viongozi mbalimbali  kutoka chama Taifa,Kibaha Vijijini pamoja viongozi wa Jumuiya ya wazazi tawi, kata, wilaya na Mkoa wa Pwani.

Katika ziara hiyo Jumaa alitembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo hospitali ya Wilaya ya Kibaha Vijijini, Zahanati na miradi mingine mbalimbali huku akisema kufanikiwa kwa miradi hiyo kunatokana na juhudi za Rais Samia.

Amesema Rais Samia katika kipindi cha miaka miwili, matunda yameonekana kwakuwa anafanyakazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo na Kibaha Vijijini miongoni mwa wilaya zilizonufaika kwa kupata fedha nyingi kutoka kwa rais.

Jumaa amesema wakati Rais Samia anaingia madarakani baadhi ya watu waliongea maneno mengi wakisema hatawezi lakini rais amewadhihirishia wananchi kuwa anaweza ndio maana kazi inaonekana .

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.

Amesema wengi walidhani miradi mikubwa itakwama lakini rais ameonyesha uhodari mkubwa na sasa mambo yanafanyika hasa katika kukamilisha Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere linalojengwa wilayani Rufiji, ambalo kasi yake ni kubwa.

“Rais wetu Dk. Samia Suluhu Hassan hakika anafanyakazi kubwa na ushahidi unaonekana, Bwawa la Mwalimu Nyerere kazi inaendelea kufanyika,madaraja makubwa  yanajengwa, barabara, afya vyote vinafanyika kwahiyo nchi inakwenda vizuri,” amesema Jumaa.

Jumaa amesema kuwa kazi kubwa inayotakiwa kufanyika ni kuhakikisha wana-CCM, wananchi na jamii nzima wanamuunga mkono rais ili haweze kufanya mambo makubwa zaidi hapa nchini.

Kuhusu Jumuiya ya Wazazi, Jumaa amesema tayari wameweka mipango na mikakati mikubwa kuhakikisha Jumuiya hiyo inaimarika hasa katika masuala ya kiuchumi jambo ambalo litafanya jumuiya ijitegemee wenyewe.

“Sasa hivi Jumuiya yetu ipo katika mashindano na UWT, UVCCM ambazo zipo juu lakini nasisi tunataka kuifanya jumuiya yetu ya Wazazi kuwa kinara kama wenzetu na hilo linawezekana lakini kikubwa Kila mmoja wetu ajitoa kusaidia kutimiza malengo,” amesema.

Jumaa amesisitiza viongozi wa CCM pamoja na wanachama kuendelea kushirikiana na jumuiya kwa ajii ya kujipanga na uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika mwaka 2024 kwani kushinda uchaguzi huo ni ishara ya ushindi wa mwaka 2025.

Mwenyekiti wa CCM Kibaha Vijijini, Mkali Kanusu, amesema chama lipo imara na kinaendeelea kushirikiana na jumuiya katika kuhakikisha kinaendelea kuchukua dola ifikapo mwakani na hata uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Pwani, Jackson Kituka, amepongeza hatua ya Jumaa kuanza ziara katika Wilaya ya Kibaha na kusema Jumuiya inaimani kubwa juu ya Mnec huyo na kuahidi kutoa ushirikiano kwake.

Kituka,amemuomba Jumaa kuwa balozi wao kwa Rais Samia kwakuwa wanaona kazi anayofanya ni kubwa huku  akisema wapo tayari kuhakikisha rais anashinda uchaguzi wa mwaka 2025 ili aweze kutimiza malengo yake ya kuwatumikia Watanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles