MNANGAGWA AMKARIBISHA TRUMP ZIMBABWE

DAVOS, USWISI


RAIS mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, amesema pamoja na kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump aliyataja mataifa ya Afrika kama yanayonuka, atamkaribisha kuwekeza hasa katika ujenzi wa viwanja vya golf.

Mnangagwa alisema hayo mjini hapa, anakohudhuria Kongamano la Uchumi wa Dunia (WEF) wakati alipokuwa akijibu maswali kuhusu matamshi ya kejeli ya Trump yaliyoripotiwa mapema mwezi huu.

Mnangagwa pia aliahidi kukubali matokeo ya uchaguzi wa mwezi Julai iwapo atashindwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here