24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

MFANYABIASHARA KIZIMBANI KWA KUDANGANYA FEDHA ALIZOKUWA NAZO

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM -

MFANYABIASHARA Boniface Mbilinyi (32) aliyekutwa na fedha nyingi Uwanja Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, amefikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kudanganya kiasi cha fedha alichokuwa nacho.

Mshtakiwa huyo alifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa, alidai mahakamani hapo kuwa Januari 13, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mshtakiwa huyo wakati akisafiri kutoka nje ya Tanzania, alitoa tamko hilo la uongo kuhusu kiasi cha fedha alichokuwa nacho.

Wakili Mbagwa alidai kuwa mshtakiwa huyo alitamka uongo kuwa ana kiasi cha dola 40,000 wakati ukweli alikuwa na kiasi cha dola 123,000.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa …………………….

Kwa habari zaidi jipatie Gazeti lako la MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles