23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

MKUU WA WILAYA AWAHAMASISHA VIJANA

FLORENCE SANAWA-MTWARA

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amewahamasisha vijana wilayani humo, kuchangamkia fursa ya urasimishaji ujuzi inayotolewa na Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE).

Akizungumza wakati wa mahafali ya pili ya mradi huo unaosimamiwa na VETA, Mmanda alisema kutokana na nguvu walizonazo vijana, wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo  kwa kufanya kazi kwa kushirikiana ili waweze kuondokana na tatizo la ajira nchini.

Alisema mradi huo umekuwa ukiwapa ujuzi vijana kufanya shughuli za kiuchumi na kuwajengea uwezo katika stadi mbalimbali zinazowapunguzia tatizo la ajira.

“Huu mradi ni mzuri na unafurahisha. Haya ni matokeo ya mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi na kuwajengea uwezo katika stadi mbalimbali za kazi.

“Hata ukiangalia vijana wengi ni wale wanaoishi maisha ya chini na wenye kipato kidogo. Kwa hiyo, ujio wa mradi huu utawasaidia kuboresha maisha yao wakiwamo wasichana na walemavu kwa kuwa ndiyo wanaopewa kipaumbele ili waweze kutumia ujuzi wao na kuleta tija ndani ya jamii,” alisema Mmanda.

Naye Mratibu wa Mafunzo, Nurdin Amri, alisema mradi huo umeshawafikia zaidi ya vijana 1500 katika Wilaya ya Mtwara.

“Katika mradi huu, wanaonufaika ni vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 35, kwani lengo ni kufikia wanaotoka katika mazigira hatarishi, mazingira magumu na wenye kipato duni,” alisema Amri.

Naye mmoja wa washiriki wa mradi huo, Habiba Shaibu ambaye ni mkazi wa Mmingano, Manispaa ya Mtwara Mikindani, alisema vijana wanapaswa kujitokeza ili wapate ujuzi utakaowafanya waweze kujiajiri wenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles