27.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

‘Miswada sheria za uchaguzi haitachakachuliwa’

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Serikali imewahakikishia wadau wa demokrasia kuwa itazingatia maoni yote yatakayotolewa wakati wa kujadili miswada ya sheria za uchaguzi na mswada wa sheria ya vyama vya siasa na kusisitiza hakuna kitakachochakachuliwa.

Miswada hiyo ilisomwa bungeni kwa mara ya kwanza Novemba 2023 na sasa wadau mbalimbali wanatoa maoni yanayolenga kuiboresha.

Hakikisho hilo limetolewa Januari 3,2024 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenister Mhagama, wakati wa mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa kujadili miswada ya sheria za uchaguzi na muswada wa sheria ya vyama vya siasa.

Washiriki wa mkutano maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa unaojadili miswada ya sheria za uchaguzi na muswada wa sheria ya vyama vya siasa.

“Watakaopewa kazi ya kuratibu maoni yawasilishwe panapohusika bila kuchakachuliwa, hata sisi Serikali tunapenda tupate nafasi ya kujifunza wadau wa demokrasia wanafikiri nini katika kuimarisha demokrasia ndani ya nchi yetu,” amesema Mhagama.

Akifungua mkutano huo Makamu wa Kwanza wa Rais katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema mkutano huo usitumike kuwasilisha msimamo wa kitaasisi bali uhakikishe maoni ya kila mdau yanazingatiwa.

“Tutoe mapendekezo yatakayopelekea kutungwa kwa sheria bora zitakazodumu kwa muda mrefu, tuwe za fikra pevu za kuona mbali ili tusije tukatunga sheria itakayolazimu mwakani turudi hapa kutoa maoni na kuifanyia marekebisho,” amesema Othman.

Amesistiza sheria zitakazotungwa ziwe chachu ya kuimarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Akiwasilisha mada kuhusu muswada wa sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi, Dk. Avemaria Semakafu kutoka (TWCP Ulingo), amesema kuna matatizo makubwa ya unyanyasaji na kupendekeza viongezwe vipengele vitakavyoleta amani na utulivu kwa wanawake ili wakiingia katika siasa waweze kulindwa.

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, amesema kutakuwa na sekretarieti itakayoratibu maoni yatakayotolewa na kuwaomba wadau waiamini huku akisisitiza kuwa hakuna kitakachochakachuliwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles