29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Miliano Pacis, msanii anayeipaisha Togo Marekani aachia ‘Queen of My Heart’

Missouri, Marekani

BARA la Afrika limebarikiwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji ambao wanafanya sanaa zao ndani na nje ya bara hili kwa hatua za mafanikio mbalimbali.

Miongoni wa vijana hao in Maxwell Pacis a.k.a Miliano Pacis, mwanamuziki aliyezaliwa Mei 5, 1993 huko Lome nchini Togo akiwa anafanya muziki wa Afropop na Jazz huku akiweza kupiga ala za muziki kama kinanda, violin na nyinginezo.

Miliano ambaye kwa sasa ni mkazi wa Saint Louis, MISSOURI nchini Marekani alifanya maamuzi ya kusoma muziki (Music Perforent) katika Chuo Kikuu cha Linden Wood ili kuwa mwimbaji huru wa Opera.

Kwa bahati mbaya mnamo 2013, Miliano alishindwa kuachia kazi alizowaahidi mashabiki kwa sababu za kiafya.

Hali hiyo ilimuweka nje ya muziki kwa muda mrefu na aliamua kuanza tena shughuli za muziki mwaka 2018 kwa kujiunga na bendi ya Jazz ambayo hakudumu nayo sana.

Kutokana na janga la corona lililoikumba dunia yote mwaka 2020, kulikuwa na uhaba wa matamasha na mashabiki wengi walilazimika kutulia majumbani hivyo Miliano hakupata nafasi ya kutumbuiza kama alivyokuwa amepanga lakini hakukata tamaa na aliendelea kusimamia kauli mbiu yake ya ‘maisha yanapokupa ndimu, tengeneza kinywaji lemonade’.

“Siku zote moyo wangu unaguswa zaidi ninaposikia mirindimo ya muziki wa Afro na Jazz hivyo hata nilipokuwa mbali na bendi yangu sikuacha kuboresha kile kitu ambacho Mungu ameweka ndani yangu kuhusu muziki,” amesema Miliano.

Miliano anasema anatamani kuufanya ulimwengu utetemeke kupitia muziki wake, akishawishiwa sana na wafaransa aliokuwa anawasikiliza akiwa mtoto pamoja na muziki wa Jazz ambao unaonyesha sura zote za maisha.
Wimbo wake wa kwanza kabisa uliitwa My Wifey na ngoma anayotamba nayo kwa sasa inaitwa Queen Of My Heart aliyomshirikisha msanii 15 Cent.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles