26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Michel Platini akamatwa Ufaransa

NANTERRE, UFARANSA

RAIS wa zamani wa chama cha soka barani Ulaya (Uefa), Michel Platini amekamatwa na kuhojiwa na maafisa wa kuzuia na kupambana na rushwa nchini Ufaransa kwa tuhuma za kuwapa Qatar uwenyeji wa michuano ya Kombe la dunia 2022.

Waendesha mashtaka wamedai wanamchunguza kiongozi huyo kwa kutuhumiwa kujihusisha na masuala ya ufisadi pamoja na kupokea hongo.

Platini, mwenye umri wa miaka 63, alikuwa kiongozi wa shirikisho hilo la soka Ulaya tangu mwaka 2007 hadi alipoondolewa madarakani mwaka 2015 kwa kukiuka maadili.

Platini ambaye aliwahi kuwa mchezaji katika nafasi ya kiungo wa timu ya taifa Ufaransa na mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon d’Or, amekana kufanya makosa hayo.

Qatar iliishinda Marekani Australia, Korea Kusini na Japan mwaka 2010 katika ombi la kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ya kombe la dunia mwaka 2022.

Platini anahojiwa huko Nanterre katika kitongoji kilichopo magharibi mwa mji mkuu Paris nchini Ufaransa.

Kiongozi huyo alitangaza kujiuzulu nafasi yake Mei 2016 mara baada ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa kipindi cha miaka minne hadi sita.

Maafisa hao wa kuzuia na kupambana na rushwa wamekuwa wakichunguza tuhuma za ufisadi zinazohusiana na kombi la dunia tangu mwaka 2018 na lijalo 2022 kwa miaka miwili iliyopita na kuna taarifa kwamba walimhoji aliyekuwa rais wa shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), Sepp Blatter mwaka 2017.

Platini alikumbwa na kashfa ya kupokea rushwa ya pauni milioni 1.3 kuoka kwa aliyekuwa rais wa Fifa, Blatter, ambaye pia alipigwa marufuku kutoshirikia soka kwa kuhusika katika suala hilo.

Hata hivyo, Blatter na yeye alikataa tuhuma hizo za kutoa kiasi hicho cha fedha kwa rais wa Uefa. Kifungo cha Blatter kilikuwa cha miaka minane, lakini baada ya kukata rufaa akapunguziwa hadi kufikia miaka minne ambapo itamalizika Oktoba 2019.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles