27.3 C
Dar es Salaam
Monday, December 4, 2023

Contact us: [email protected]

SIMBA YAMNASA BEKI KISIKI SINGIDA UNITED

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Simba imemsajili kwa mkataba wa miaka miwili, beki Kennedy  Juma.

Simba imemsajili Juma, akiwa mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake katika kikosi cha Singida United, alichokisaidia kumaliza msimu katika nafasi ya 13, baada ya kukusanya pointi 46.

Juma anakuwa mchezaji mpya wa pili, kutua Msimbazi, baada ya Wekundu hao kufanikisha  usajili wa kipa Beno Kakolanya aliyemaliza mkataba wa kuichezea Yanga.

Simba pia imetangaza kurefusha mikataba ya baadhi ya nyota wake waliokuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha timu hiyo msimu uliopita wa  Ligi Kuu Tanzania  Bara na Ligi ya Mabingwa,  ambapo kilifikia hatua ya  robo fainali.

Wakali hao ni mabeki Erasto Nyoni, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, kiungo Jonas Mkude, washambuliaji Meddie Kagere, John Bocco na kipa Aishi Manula.

Kwa mujibu wa mtandao rasmi wa klabu hiyo, Juma anategemewa kuifanya safu ya  ulinzi ya Simba kuwa imara zaidi, wakati ikisubiri kushiriki Ligi Kuu msimu ujao na Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Juma amesaini mkataba wa miaka miwili, ataungana na wachezaji wengine waliopo kwa kuisaidia safu ya ulinzi kuwa imara zaidi na kuleta ushindani,” ilielezea taarifa ya klabu hiyo.

Mabeki wengine wanaunda safu ya ulinzi ya kikosi cha Simba ni Pascal  Wawa ambaye mkataba wake umefikia tamati, kama ilivyo kwa Jjuuko Murshid, Paul Bukaba na Yusuph Mlipili.

Uongozi wa Simba chini ya mwekezaji wake, Mohamed Dewji, umeweka wazi nia yao ya kutaka kufanya vizuri zaidi ya msimu uliopita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mo amewaambia  mashabiki wa klabu hiyo kuwa, yupo tayari kutoa fedha ili kufanikisha usajili mchezaji yeyote mkali,ili kuhakikisha Wekundu hao wanaiteka Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles