27.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Miaka 60 ya Uhuru| Tanzania ilivyounganisha mtandao wa barabara

*TRC kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa SGR

*Madaraja yaimarishwa kila pembe ya nchi

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) ipo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi wa reli ya SGR awamu ya pili kwa kipande cha Tabora – Kigoma (Km 411), Kaliua-Mpanda-Karema (Km 321), Keza – Ruvubu (km 36); Isaka – Rusumo (km 371), na Uvinza-Musongati (Km 240).

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ijumaa jijini Dodoma kuhusu mafanikio ambayo imeyapata wizara hiyo ndani ya kipindi cha miaka 60,Waziri Mbarawa amesema amesema serikali kupitia TRC ipo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi wa reli ya SGR awamu ya pili kwa kipande cha Tabora – Kigoma (Km 411); Kaliua-Mpanda-Karema (Km 321), Keza – Ruvubu (km 36); Isaka – Rusumo (km 371), na Uvinza-Musongati (Km 240).

“Upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa vipande hivi umekamilika na hatua inayoendelea ni kuandaa makabrasha ya zabuni,”amesema Prof. Mbarawa.

UJENZI WA MADARAJA

Waziri Mbarawa amesema katika kipindi cha miaka 60 ya Uhuru, serikali pia imejenga madaraja makubwa na madogo nchini.

Amesema madaraja makubwa yaliyokamilika ni pamoja na daraja la Kirumi (Mara), daraja la Mto Kagera (Kagera), daraja la Rusumo (Kagera), daraja la Mkapa (Pwani), daraja la Umoja (Mtwara), daraja la Kikwete (Kigoma), daraja la Sibiti (Singida), daraja la Mara (Mara), daraja la Mlalakuwa (Dar es Salaam).

Mbarawa ameyataja mengine kuwa ni daraja la Momba (Rukwa), Lukuledi II (Lindi), Ruhuhu (Ruvuma/Njombe), Magufuli (Morogoro), Magara (Manyara), Nyerere (Dar es Salaam), Kavuu (Katavi), Ruvu Chini (Pwani) na mengine mengi.

Daraja la Mwalimu Julias Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Amesema Madaraja makubwa yanayoendelea kujengwa ni pamoja na daraja la Tanzanite (Dar es Salaam), Msingi (Singida), Daraja Jipya la Wami (Pwani), Kitengule (Kagera), Gerezani (Dar es Salaam) na Kigongo – Busisi (Mwanza). Aidha, mengine 7 yapo kwenye hatua ya usanifu ya ujenzi. Madaraja hayo ni Sukuma (Mwanza), Simiyu (Mwanza), Mkenda (Ruvuma), Mtera (Dodoma/Iringa), Godegode (Dodoma), Malagarasi Chini (Kigoma) na Ugalla (Tabora) yako kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

BARABARA

Waziri huyo amesema mafanikio yaliyopatikana katika mtandao wa barabara tangu kupata uhuru mwaka 1961 ni kuongezeka kwa mtandao wa barabara za lami kutoka kilometa 1,360 (1961) hadi kufikia kilometa 11,186 (Septemba 2021) na hivyo kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mfano ni kwa wakazi wa kanda ya ziwa ambao walikuwa wanatumia zaidi ya saa 30 kusafiri kwa kutumia usafiri wa mabasi kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na wakati mwingine kulazimika kupitia nchi jirani kama vile Kenya (Nairobi), ambapo kwa sasa wasafiri wanatumia chini ya saa 15 kwa safari hiyo,”amesema Prof. Mbarawa.

Amesema katika kipindi hiki, serikali inaendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 1,593 ambazo zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Waziri huyo amesema baadhi ya miradi inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa barabara za Mzunguko wa Nje Dodoma (Dodoma Outer Ring Road) kilometa 112.3, Tabora – Koga – Mpanda kilometa 365.98 na Kabingo – Kibondo Town – Kasulu – Manyovu kilometa 286.5.

KUUNGANISHA MAKAO MAKUU YA MIKOA KWA LAMI

Aidha, Waziri Mbarawa amesema sera ya serikali ni kuunganisha makao makuu ya mikoa yote nchini, ambapo hadi sasa yote imeungwa kwa barabara za lami isipokuwa michache ambayo hata hivyo serikali inaendelea kutekeleza miradi ya barabara ya kuunganisha mikoa hiyo.

Amesema miradi inayoendelea kutekelezwa kwa sasa ni pamoja ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Tabora – Usesula – Komanga – Kasinde – Mpanda (km 365.98) inayounganisha mikoa ya Katavi na Tabora, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Njombe – Ndulamo – Makete (km107.4), inayounganisha mikoa ya Njombe na Mbeya.

“Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Makutano – Natta (sehemu ya Makutano – Sanzate (km 50) na sehemu ya Wasso (Loliondo) – Sale Jct (km 49) kwa ajili ya kuunganisha mikoa ya Mara na Arusha.Serikali ina mpango wa kuanza ujenzi wa sehemu ya Mkiwa – Itigi – Noranga (km 56.9), kwa ajili ya kuunganisha mikoa ya Singida – Mbeya,”amesema Prof. Mbrawa.

USAFIRI WA ANGA

Waziri Mbarawa amesema serikali pia inaendelea kuimarisha usafiri wa anga ambapo Viwanja vya ndege vyenyelengo la kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji vimeendelea kujengwa na kukarabatiwa katika mikoa mbalimbali nchini.

Amesema hadi sasa Serikali ina jumla ya Viwanja vya Ndege 58 vilivyo chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) na kimoja kilicho chini ya KADCO.

Ameitaja miradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kuwa ni  pamoja na ule wa Jengo la tatu la kisasa la abiria (TB – III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere limejengwa;Uboreshaji wa Viwanja vya Ndege vya Mwanza (Phase I), Tabora (Phase II), Kigoma (Phase I), Bukoba (Phase I), Dodoma, Mpanda na Mafia ambavyo vimekalimika kwa kiwango cha lami.

“Ukarabati wa viwanja vya Ndege vya Mtwara, Iringa, Songwe, Geita, Songea na Musoma upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji;Mkataba wa Ujenzi wa mradi mpya wa Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato Awamu ya kwanza (package 1) unaohusisha ujenzi wa miundombinu ya Kiwanja (Airport Infrastructure,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles