24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Mhasibu Amcos atiwa mbaroni kwa biashara ya magendo

Yohana Paul, Mwanza

TAASISI  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza inamushikilia Mhasibu wa Chama Cha Ushirika (Amcos) cha Mhedi cha wilayani kishapu mkoani Shinyanga, Paul Nkuba pamoja na wafanyabiashara 13 na madalali watatu kwa kosa la kujihusisha na biashara ya magendo ya dawa za kilimo.

Akitoa taarifa mwishoni mwa wiki jijini hapa,  Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Stenga alisema mhasibu huyo ambaye ni maarufu kwa jina la Nchimika amekuwa akisafirisha na kuuza dawa za kilimo kutoka kwenye Amcos hiyo  na Amcos zingine na kuzileta Mwanza kwa madalali na wafanyabiashara wa maduka ya pembejeo na kilimo Mtaa wa Lumumba jijini Mwanza.

Stenga alitanabaisha kuwa dawa hizo ambazo zimekuwa zikifanyiwa ubadhirifu ni dawa zilizonunuliwa na serikali na kupelekwa bodi ya pamba kwa lengo la kupatiwa wakulima wa pamba kupitia vyama vya Msingi na Ushirika (Amcos).

Alisema baada ya kupata taaarifa hiyo Takukuru walifanya uchunguzi na upekuzi kwenye maduka hayo ya pembejeo na kukuta dawa zenye thamani ya Sh millioni 12.6 ambazo walipaswa kupatiwa wakulima kwenye amcos zao zikiwa zinauzwa kinyume cha utaratibu.

“Takukuru Mwanza ilifanya ufuatiliaji kwenye Amcos zote na kubaini changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba ni pembejeo kutowafikia wakulima wa pamba kwa wakati na ucheleweshaji wa malipo ya wakulima baada ya mauzo.

“Baada ya kubaini tatizo hilo Takukuru ilifanya ufuatiliaji na kujiridhisha kuwa baadhi ya viongozi wa Amcos wasio waaminifu ikiwemo mhasibu huyu tuliyemkamata wamekuwa wakifanya biashara ya magendo ya dawa hizo muhimu kwa wakulima na kusababisha wakulima kukosa jambo ambalo  ni kosa kisheria.

“Pia kwa muda mrefu Takukuru imekuwa ikifuatilia madeni ya wakulima wa vyama vvya Amcos na imeweza kuokoa fedha nyingi ambazo zimehujumiwa na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo wasio waaminifu na kuwasababishia wakulima kuhangaikia malipo yao kwa muda mrefu bila mafanikio,” alisema Stenga.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles