25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Mgunda apigia hesabu nafasi tano mapema

MOHAMED KASSAR -DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema licha ya ushindani mkali utakaokuwepo katika Ligi Kuu Tanzania msimu ujao, kikosi chake kitapambana kuhakikisha kinamaliza ndani ya nafasi tano za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Coastal ilimaliza msimu uliopita, ikiwa katika nafasi ya nane, baada ya kujikusanyia pointi 48, kwenye michezo 38 walioshuka dimbani.

Wagosi hao wa Kaya watafungua pazi la Ligi Kuu Bara msimu msimu ujao, kwa kuvaana na Polisi Tanzania, katika mchezo utakaochezwa Agosti 24, mwaka huu, Uwanja wa Ushirika Moshi, Kilimanjaro.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mgunda alisema mipango yake ni kujenga kikosi cha ushindani kitakachomuwezesha kukusanya pointi za kutosha ili kumaliza ndani ya nafasi tano za juu kwenye ligi.

Alisema kikosi chake kimeimarika zaidi kutokana na kunasa wachezaji wenye uwezo, ambao kwakuwaunganisha na waliopo wataisadia timu hiyo kufikia lengo lao hilo.

“Tunaendelea vizuri kujipanga kwa ajili ya msimu ujao, kila kitu kinakwenda, wachezaji tayari wameiva kiasi cha kutosha, tunafahamu utakuwa msimu mgumu kutokana kuongezeka kwa ushindani, lakini tumejipanga kukabiliana na changamoto hiyo.

“Nina kikosi kizuri tofauti na msimu uliopita, kwa vijana nilionao nina imani kubwa tutafanya vizuri, lengo letu ni kusogea juu kwa nafasi tatu au zaidi kutoka pale tulipoishia msimu uliopita,”alisema Mgunda.

Coastal Union ilimaliza nafasi ya nane, ikiwa na pointi 48, katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles