30.2 C
Dar es Salaam
Friday, May 3, 2024

Contact us: [email protected]

Mgomo wa wafanyakazi wavuruga safari za ndege Nairobi

NAIROBI, KENYA

HUDUMA za usafiri wa ndege zimevurugika na abiria kukwama katika uwanja mkuu wa ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) mjini hapa, huku baadhi ya ndege zikielekezwa kutua katika nchi jirani ya Tanzania.

Mgomo huo ambao uliitishwa na Muungano wa Wafanyakazi (KAWU) unachagizwa na kupinga mpango wa kulifanya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kusimamia shughuli za JKIA kwa kipindi cha miaka 30.

Wabunge pia wamekuwa wakipinga mpango huo, ambao pia unaiunganisha Mamlaka ya Usimamizi wa Viwanja vya Ndege (KAA).

Wengi wa wasafiri katika uwanja huo wenye shughuli nyingi zaidi za ndege kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika walikumbana na zogo la mgomo wa wafanyakazi bila kutarajia.

Mgomo huo ulioanza usiku wa manane, umeathiri pia shughuli katika viwanja vya ndege vya miji ya Mombasa, Kisumu na Eldoret kutokana na ndege kushindwa kusafiri kwa wakati.

“Wafanyakazi wanaopinga usimamizi wa JKIA kutwaliwa na KQ walisema uamuzi huo huenda ukachangia wengi wao kukosa ajira,” alisema Katibu Mkuu wa KAWU, Moses Ndiema kabla ya kukamatwa na polisi.

Shirika la Ndege la Kenya lina mipango ya kuingia ubia na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ili kuvisimamia.

Mapema wiki hii, Waziri wa Uchukuzi, James Macharia alikanusha madai kuwa KQ inaendesha ndege zinazosimamiwa na baadhi ya watu wanaopanga kuchukua usukani wa viwanja vya ndege nchini.

Wafanyakazi wanaogoma wanataka usimamizi wa KQ na KAA ubadilishwe.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Shirika la Ndege la Kenya, limeonya wasafiri watarajie matatizo ya usafiri siku nzima ya jana.

KAWU imehoji ni vipi Shirika la Ndege la Kenya lichukue usimamizi wa KAA ilhali limekuwa likipata hasara ya mabilioni ya fedha kila mwaka.

Muungano huo unasema kuwa hatua hiyo itachangia hasara ya mabilioni ya fedha huku wafanyakazi wengi wakipoteza ajira.

Kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, Katibu Mkuu Mtendaji wa KQ, Sebastian Mikosz, Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Michael Joseph na wakurugenzi kadhaa walilipwa dola milioni 13, hali inayotiliwa shaka na KAWU.

Wanataka vigogo hao kutimuliwa kwa ubadhirifu wa fedha.

Serikali inamiliki asilimia 46.5 ya hisa katika KQ huku benki 11 zikimiliki asilimia 35.6

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles