29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

Wabunge Democratic waanzisha uchunguzi mpya dhidi ya Trump

WASHINGTON, MAREKANI

WABUNGE wa Chama cha Democratic nchini hapa wameanzisha uchunguzi mpya dhidi ya Rais Donald Trump, ambao unatishia kumzonga hadi msimu wa uchaguzi wa mwaka 2020.

Uchunguzi huo unahusisha shughuli za Ikulu (White House), kampeni na biashara za familia yake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria ya Bunge la Marekani, Jerrold Nadler alisema jopo lake linaanza uchunguzi kuhusu uwezekano wa kuzuiwa haki, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Na amekusanya nyaraka kutoka kwa watu 81 wanaohusishwa na Trump na washirika wake.

“Kamati ya Sheria ya Bunge imetuma maombi ya stakabadhi kwa watu 81, ambao wana taarifa zinazohusu uchunguzi wetu wa matumizi mabaya ya madaraka na uhalifu mwingine ambao unaweza kuwa umetendeka White House,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo, Jamie Raskin.

Uchunguzi huo mpana huenda ukatoa nafasi kwa juhudi za kumwondoa madarakani Rais Trump ingawa viongozi wa chama cha Democratic wameapa kuwa wataangazia njia zote na kuitathmini ripoti ya wakili maalumu, Robert Mueller kabla kuchukua hatua yoyote ile.

wana-Democratic walichukua udhibiti wa Bunge la Wawakilishi na tayari wameanza kutumia mamlaka yao kumwekea shinikizo rais.

Trump amezungumza na wanahabari baada ya tangazo la uchunguzi huo na kusema atashirikiana na wanaofanya uchunguzi huo.

“Kila wakati nashirikiana na kila mmoja. Unajua, uzuri ni kwamba yote haya ni uongo mtupu,” alisema Trump.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders alidai kuwa uchunguzi huo ni wa aibu na kudhalilisha kuhusiana na mambo ya uongo.

Alidai kuwa Nadler na wa-Democratic wenzake wameanzisha uchunguzi huo wa uongo kutokana na hofu kuwa jambo walilokuwa wakilisema kwa miaka miwili la Trump kushirikiana na Urusi kushinda uchaguzi, kwa sasa linaanza kukosa mashiko.

Majina hayo 81 yaliyoko kwenye orodha ya kamati hiyo yote yanagusia maisha ya Trump kuanzia Ikulu, biashara, kampeni yake na kamati iliyosimamia kipindi cha mpito kutoka kampeni hadi urais.

Kamati hiyo pia inalitaka Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI), Wizara ya Sheria na nyinginezo kuwasilisha stakabadhi zinazohusu kuachiwa kwa wakili wa zamani wa Trump, Mchael Cohen, aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa, Michael Flynn na mwenyekiti wa zamani wa kampeni ya Trump, Paul Manafort.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles