30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

MGOMBEA CCM AKAMATWA AKIGAWA RUSHWA

Hadija Omary, Lindi

Mgombea wa nafasi ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kilangala, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Jenga Mohamedi  na wajumbe saba wa Mkutano Mkuu wa kata wa chama hicho wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakidaiwa kupokea na kutoa rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 18, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Steven Chami amesema watu nane wamekamatwa akiwamo Mgombea ukatibu aliyekutwa akitoa rushwa kwa wajumbe ili achaguliwe.

Kwa mujibu wa Chami, tukio hilo limetokea jana saa mbili asubuhi kwenye eneo la uchaguzi huku watuhumiwa wakiwa  na fedha Sh 2,000  kila mmoja huku mpambe wa mgombea huyo alikutwa na bulungutu kiasi hicho cha fedha zenye thamani ya Sh 50,000 na orodha ya majina ya wajumbe wa mkutano huo.

Alisema watuhumiwa wanashikiliwa  na Taasisi hiyo hadi mahojiano yatakapo kamilika na hatua zingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles