26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

WANAHISA CRDB: DK. KIMEI ‘MTAMU’


ELiya Mbonea, Arusha  |

Wanahisa wa Benki ya CRDB, wamesema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk.Charles Kimei ni ‘mtamu’ ndiyo maana kila mtu anamuhitaji ambapo wamemtaka asiondoke licha ya muda wake kumalizika mwakani.

Taharuki kwa wanahisa hao imejitokeza leo katika Mkutano wa Mwaka wa Wanahisa wa benki hiyo, unaofanyika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC).

Akiwasilisha taarifa yake ya mwaka kwa wanahisa, Dk.Kimei pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kuwaambia wanahisa kwamba muda wake wa utumishi CRDB utamalizika Mei 2019.

Kutokana na hali hiyo, wanahisa hao wamesema wanafanya ushawishi kwa kumwandikia barua Rais Dk.John Magufuli,amuache Mkurugenzi huyo aendelee kutumikia benki hiyo kwa miaka mitano mbele kwani wanaamini aliwavusha Mto Yordani vivyo hivyo wanaamini atawafikisha Yerusalem.

Baadhi ya wanahisa waliochangia taarifa za Benki hiyo waliendelea kumuomba Dk.Kimei asiondoke kwani ndiye mwenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kushawishi hata wa kwenda kumuona Rais Magufuli.

“Sisi tunaweza kuwa watu wa ajabu, mkubwa wa nchi amemsifu Dk.Kimei, sisi ni nani hadi tumuache aondoke?” alisema mmoja wa wanahisa hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles