23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mgodi waporomoko Simiyu, waua na kujeruhi

Na Derick Milton, Bariadi

Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kufukiwa na shimo katika machimbo ya dhahabu yaliyopo kijiji cha Halawa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mtanzania Digitala Julai 4, 2022 Afisa Madini wa Mkoa, Amini Msuya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo ameeleza moja ya mashimo katika mgodi huo liliporomoka wakati linatengenezwa.

Amesema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, majira ya saa 7 na saa 8 Usiku, huku akitaja mmiliki wa mgodi huo kuwa ni John Stephano Luhende and Pettiness.

Amesema kuwa katika mgodi huo ambao ulikuwa na wiki mbili tangu ugunduliwe, mashimo mawili yalikuwa yanakarabatiwa kutokana na kuwa katika hali ambayo siyo nzuri.

Amesema wakati mashimo hayo yanaendelea kukarabatiwa, ndipo moja likaporomoka na kuwafukia wasaidizi wa mafundi ambao walikuwa ndani wanaendelea na ukarabati.

“Kati ya hao watatu mmoja amefariki, lakini wengine wawili walijeruhiwa na tulikuwakimbiza hospitali kwa ajili ya kupata matibabu na mpaka sasa hali zao zinaendelea vizuri,” amesema Msuya.

Amesema kuwa wakati ukarabati ukiendelea, gema la shimo hilo liliporomoka na kuwafunika ambapo ameeleza licha ya tukio hilo kutoa shughuli za uchimbaji zinaendelea hasa kuendelea kujengwa kwa mashimo hayo.

“Ajali za migodini kama hizi ni mambo ya kawaida hasa hasa wakati wa ujenzi wa maduara, hivyo kwa sasa shughuli za uchimbaji zinaendelea na wala hatujafunga mgodi na yale maduara yanaendelea kukarabatiwa,” ameeleza Msuya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles