28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

TIRA, NIC kuwafikia wakulima, Wavuvi

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

KAMISHINA wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware amesema Serikali ipo tayari kushirikiana na Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwa kuhakikisha inawafikia wakulima, wafugaji, na wavuvi wote nchini.

Dk. Saqware ameyasema hayo alipotembelea katika banda la NIC lililopo katika Maonesho ya Biashara ya kimataifa 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.

Amesema serikali imekuwa ikitegemea sana Shirika la NIC katika kuendeleza soko katika maeneo ya bima ya kilimo, majengo, pamoja na bima mbalimbali.

Dkt Sqware amesema NIC ni wazoefu zaidi katika soko la bima kutokana na kwani wamekuwa na mtaji mkubwa na wataalamu wa kutosha katika soko.

“Ukizungumzia bima Tanzania hakuna namna unaweza kuisahau NIC kwa maana ya wataalamu, uzoefu pamoja na mtaji,” amesema Dk. Sqware

Vilevile amesema hivi karibuni NIC wamejikita katika bima ya kilimo ambapo amewapongeza kwa hatua hiyo na kuhaidi kuendelea kushirikiana nao.

“Tayari tumewapatia namba viongozi wa NIC ili waweze kuwasiliana na viongozi wa wakulima na wafugaji hapa nchini ili waaze kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuwafikia zaidi na kuwapatia bima

Naye Mkurungezi wa Masoko na huduma kwa wateja NIC, Yesaya Mwakifulele amesema katika Maonesho hayo NIC imejikita katika ushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha inatoa huduma mbalimbali kuhusu suala nzima la bima.

Amesema katika Maonesho hayo wamekuja na APP ya NIC kigajani ambayo inamuwezesha mteja kupata huduma akiwa nyumbani bila ya kufika katika ofisi zao.

“Kupitia APP hiyo mteja anaweza kujihudumia kwa hatua chache tu ambayo ataweza kukata bima ya aina mbalimbali ikiwemo nyumba, gari.

Akizungumzia kuhusu suala nzima la madai amesema NIC imekuwa ikifanya ulipaji huo ndani ya siku saba tu iwapo taarifa zote zikiwa sawa.

“Kwa sasa hatuna madai yoyote ambayo ayajalipwa labda yale ambayo taarifa zake aziko sawa,” amesema Mwakifulele

Aidha amewataka watanzania wote kwa ujumla kufika katika banda lao ili waweze kupata elimu pamoja na huduma za uhakika za bima ambazo zitaweza kumsaidia pale anapopata majanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles