MFUMKO wa Bei Septemba mwaka huu umepungua kwa asilimia pointi 4 na kuwa asilimia 4.5 Septemba kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa Agosti mwaka huu.
Hii inamaanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Agosti, mwaka huu. Ni punguko dogo lakini ni muhimu kwa serikali iliyoko madarakani kwa kudhibiti matumizi kwa serikali.
Mfumuko wa bei kwenye vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba mwaka huu ulipungua kwa asilimia 6.0 kutoka asilimia 7. Agosti mwaka huu.
Ripoti ya mfumuko wa bei ya Septemba mwaka huu inaonesha kuwa mfumuko wa bei wa vyakula vinavyotumiwa nyumbani na nje ya nyumbani ulipungua na kufikia asilimia 6.1 katika Septemba kutoka asilimia 7 Agosti mwaka huu.
Mfumuko wa Bei, ukiondoa chakula na nishati, ulipungua kwa asilimia 2.4 Septemba, ikilinganishwa asilimia 2.6 Agosti mwaka huu na hivyo kufanya ununuzi wa shilingi 100 za Tanzania kufikiwa shilingi 97 na senti 04 katika Septemba 2016 kuanzia Desemba 2015. Ilikuwa TZS96 na 83 senti mwezi Agosti 2016. Ina maana shilingi ya Tanzania iliongezeka thamani dhidi ya fedha nyingine na hivyo kufanya watu kulalama kuwa hakuna fedha mifukoni.
Katika thamani ya Sh.100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh. 97 na senti 04 mwezi Septemba, 2016 kutoka Desemba mwaka jana, ilipokuwa Sh.96 na senti 83 mwezi Agosti mwaka huu.
Mfumuko wa bei unazidi kubadilika kwa kupanda na kushuka kutoka asilimia 6.8 Desemba mwaka jana, Aprili mwaka huu mfumuko ulishuka hadi kufikia asilimia 5.1, na ukaongezeka hadi asilimia 5.5 Juni mwaka huu, na kushuka tena na kuwa asilimia 5.1 Julai, asilimia 4.9 Agosti na asilimia 4.5 Septembi mwaka huu.
Kwa upande wa ripoti ya uchumi ya Benki Kuu (BOT) ya Agosti mwaka huu inaonesha thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma katika mwaka unaoishia Julai mwaka huu , yaliongezeka kwa asilimia 7.5.
Ripoti hiyo inaelezea mauzo ya nje kwa ujumla yalifikia dola za kimarekani milioni 9.810.4, ikilinganishwa na dola milioni 9,128.4 katika mwaka ulioisha Julai mwaka jana.
Mabadiliko hayo yalitokana na ongezeko katika sekta ya utalii, bidhaa za viwandani, na dhahabu.
Sekta ya utalii ni miongoni mwa sekta iliyoongoza katika kuleta fedha za kigeni na bidhaa za viwandani, dhahabu, na mauzo ya bidhaa asilia.
Mapato ya fedha za kigeni kutoka bidhaa za viwandani iliongezeka kwa asilimia12.6 kufikia dola za kimarekani milioni 1,448.7 kwa mwaka ulioisha Julai mwaka huu.
Ongezeko hilo nikutokana na maboresho ya sekta katika mavazi nguo (textile), mafuta ya kula, vitu vya plastiki, chuma na bidhaa za chuma.
Ripoti hiyo inaelezea pia mauzo ya nje ya madini ya dhahabu iliongezeka kwa asilimia 7.7 kufikia dola za kimarekani milioni 1,364.4 hili ni kutokana ongezeka la kiwango cha kuuza nje.
Miongoni mwa mauzo ya nje kwa bidhaa za ndani zilizoongezeka ni kama kahawa (dola milioni 151.8 ambayo ni kwa aslimia 1.3), chai (dola 48.8 asilimia10.2), karafuu (dola milioni 46.2 asilimia 52.5) na mkonge (dola milioni 25.7 40.4 ).
Pia kulikuwa na kupanda kwa thamani ya mauzo ya nje mafuta yanayotokana na mbegu za mazao, malighafi ya ngozi na kakao, nafaka, na bidhaa za mbao.