31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Mfumo mpya wa ShuleSoft wazinduliwa, matapeli waonywa

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

TAASISI inayojihusisha na mifumo ya kidigitali katika uendeshaji wa shule nchini Shulesoft, imezindua toleo jipya la mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa shule za msingi na sekondari kidigitali nchini baada ya ule wa zamani kudukuliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari  Aprili 9, 2024 jijini Dar es Salaam kwenye  uzinduzi wa toleo jipya la mfumo huo, Mkurugenzi wa ShuleSoft, Ephraim Swilla alisema wamefanya maboresho ya mfumo huo kuongezea baadhi ya vipengele ambavyo havikuwepo awali kutokana na mapendekezo ya wateja wao na kudhibiti wimbi la wadukuzi.

Alisema mfumo mpya wa ShuleSoft unajihusisha na usimamizi wa shule, kusaidia masuala ya utawala, taaluma, kifedha, mawasiliano na kurahisisha ujifunzaji kwa mfumo wa kidigitali wa ShuleSoft:

Aliongeza kuwa toleo hilo jipya limeunganisha wadau mbalimbali zikiwemo benki na mitandao ya simu kwa ajili ya  malipo shuleni na kuokoa muda kwa utawala, wazazi pamoja na wanafunzi.

“Mfumo wa toleo hilo jipya la shulesoft unakwenda kusaidia, masuala ya usimamizi wa shule katika nyanja mbalimbali ambazo ni mahudhurio, maktaba, bweni, taaluma, mawasiliano ya moja kwa moja na wazazi pamoja na uwajibikaji wa wafanyakazi,”alisema Swilla na kuongeza.

“Shule sasa wanaweza kusimamia mambo ya mahudhurio, maktaba, bweni lakini tunacho kipengele cha kutuma mawasiliano kwa wazazi tumeuunganisha na Whatsapp, Telegram ikiwepo program tumishi (aplikesheni) mpya ya simu inayoitwa (shule soft parent experience) ambapo mzazi atajua kila kitu kinachoendelea shuleni.

Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Faraja Msuya.

Aidha Swilla alitoa onyo kwa watu wanaoiba kazi za wabunifu nakufanya udanganyifu kwa shule na kuharibu ubunifu wao uliofanyika kwa kutumia jina la taasisi hiyo  na kutengeneza taswira mbaya kwa jamii kwa kujiingizia kipato kwa njia ya udanganyifu.

Mwanasheria wa Taasisi hiyo, Faraja Msuya, ametoa onyo kwa watu wanaotumia nembo ya taasisi hiyo kufanya udanganyifu na kwa atakayebainika atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Tayari mfumo huo umezinufaisha  shule za msingi na sekondari katika 470 nchini na kufungua ofisi katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mbeya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles