24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Mfanyabiashara kizimbani kwa tuhuma za kukwepa kodi ya Sh bilioni 3

NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

JAMHURI imemfikisha mahakamani Mfanyabiashara, Poison Batisha (36), kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya Sh bilioni tatu kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mshtakiwa huyo alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega na kusomewa mashtaka na  Wakili wa Serikali, Janeth  Magoho.

Katika shtaka la kwanza ambalo ni kuwepa kulipa kodi, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari mosi mwaka 2012 na Mei 12, mwaka huu katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam ambapo alikwepa kodi Sh zaidi ya bilioni tatu,  katika bidhaa zake za  kielekroniki.

Inadaiwa katika shtaka la pili mshtakiwa huyo aliisababishia TRA hasara ya kiasi hicho cha fedha baada ya kukwepa kulipa kodi.

Katika shtaka la nne ambalo ni  utakatishaji  fedha, Wakili Janeth alidai mshtakiwa alijipatia Sh 3,010, 0092,416, kwa kukwepa kodi, wakati akijua fedha hizo ni zao la uhalifu.

Mshtakiwa hakurusiwa kujibu chochote kwani mashtaka yanayomkabili ni uhujumu uchumi na upande wa mashitaka walidai upelelezi haujakamilika hivyo kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Juni 18, mwaka huu kwa kutajwa ambapo mshitakiwa alirudishwa rumande.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles