31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mfahamu Milli Izzah mkali wa ‘Jeje’ Marekani

Arizona, Marekani

HAKUNA aliyeweza kuzuia kipaji cha muziki cha Milli Izzah, Mtanzania mwenye asili ya Burundi kutokana na wazee wake ambaye alihamia nchini Marekani mwaka 2008.

Izzah amesema kipaji chake kilianza kuonekana kwenye soka na baada ya misukosuko mingi ikiwemo kumpoteza babu yake aliacha mpira wa miguu na kujikita kwenye muziki ambao anafanya mpaka sasa.
.
“Wakati wowote ninaporekodi wimbo huwa nafanya jinsi ninavyohisi, ndivyo ninavyoelezea hisia zangu,” amesema Izzah.

Watu wanapomwuliza kwanini aliacha kucheza mpira wa miguu huwa anasema: “Niliacha kwa sababu familia yangu haikuwa na pesa za kutosha kulipia ada ya timu na majaribio kwa hivyo niligeukia muziki kwa sababu haikuchukua pesa nyingi kurekodi na kutoa nyimbo,” .

Wakati Izzah akichia wimbo wake wa kwanza ‘Na Na’ mjomba wake ambaye ni Manger Eddie Bandz analiyeanzisha lebo ya Phazi alimwambia aichukulie kwa uzito kwa sababu ya mapokezi makubwa aliyopata.

Ndipo Izzah alipopata nguvu zaidi hivyo akaingia tena studio kurekodi wimbo ‘Waitin’ ambao umefanya vizuri na kutazamwa na watu elfu 34 kwenye YouTube.

Hata mhasibu wa Izzah, Mae Mae alishangaa juu ya mafanikio aliyokuwa akipata msanii huyo haswa kama msanii wa Afro nchini Marekani ambao sasa anatamani zaidi kuendelea kujifunza muziki.

Baada ya kuachia wimbo wake Jeje na kufanya vizuri, Izzah na timu yake kubwa akiwa na Flex, Bobo na promota wake Jafari wameendelea kuwa na nguvu zaidi.

“Mashabiki sasa hivi watarajie muziki zaidi na ushirikiano mkubwa kutoka kwa wasanii wengine wa kimataifa,” amesema Izzah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles