27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Meya wa Chadema ahamia CCM

NA MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

MEYA wa Manispaa ya Ilala,  Charles Kuyeko (Chadema) ametangaza  kujiuzulu nafasi hiyo na kuhamia Chama  Cha Mapinduzi (CCM)  kwa kudai kuwa  ndicho chama anachokipenda  kwa dhati .

Kuyeko ambaye pia ni diwani wa  Kata ya Bonyokwa alitangaza uamuzi huo jana ambapo pamoja na kuwashukuru viongozi wa Chadema alisema kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuvutiwa na  kazi zinazofanywa na Rais Dk.John Magufuli huku akiwashukuru .

“Kwa kipindi hiki kwa kweli niendelee kumshukuru Rais Dk.Magufuli kwa sababu anafanya kazi ya ajabu iliyotukuka,  tuendelee kumsapoti, nirudie tena kuwashukuru chama changu cha sasa Chadema ambao walinipa nafasi ya kugombea kupitia kwao.

“Na mimi sikuwadharau  niliendelea kuwaheshimu na nitaendelea kuwaheshimu kwa heshima waliyonipa lakini mimi kwa kweli mapenzi yangu ya dhati  yapo CCM kwa sababu nimekulia humo, nimeishi  humo,”alisema Kuyeko.

Alisema siku zote alikuwa akitamani Tanzania ipate rais mkali  lakini hakujua  atakuja nani  lakini bahati nzuri alitokea Rais Magufuli ambaye alikuwa akizikubali kazi zake.

 “Nilikuwa na kubali kazi yake sana akiwa waziri wa ujenzi na uchukuzi alijenga barabara nyingi na alifanya mambo mengi makubwa kila wizara aliyokwenda.

“ Rais Magufuli kwa kweli ni mtu wa kuigwa  ni mtu ambaye Mungu amempa kalama na vipawa mbalimbali vyakufanya kazi  ni lazima  tukubali kama nilivyotangulia,”alisema Kuyeko.

Alisema pamoja na kwamba alikuwa chama cha upinzani  ambacho anawaheshimu viongozi wake kwakumpa nafasi lakini hakuwahi kusema kama serikali iliyopo madarakani mbaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles