23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

MERKEL KUWANIA MUHULA WA NNE

BERLIN, UJERUMANI


German Chancellor Angela Merkel gestures

KANSELA Angela Merkel wa Ujerumani, juzi amethibitisha kuwa atagombea tena ukansela katika uchaguzi wa mwaka 2017.

Wajerumani wamekuwa wakisubiri kwa hamu kwa miezi kadhaa sasa kutaka kujua iwapo Kansela Merkel ambaye amekuwapo madarakani tokea mwaka 2005, atawania muhula wa nne au la wakati wa uchaguzi uliopangwa kufanyika Septemba mwakani.

Baada ya miezi kadhaa ya tetesi, inaripotiwa kansela huyo amewaambia wanachama wenzake wa Chama cha CDU mjini Berlin kuwa yuko tayari kukiwakilisha katika uchaguzi huo.

Kiongozi huyo wa CDU mwenye umri wa miaka 62, amekuwa akikabiliwa na changamoto katika miezi ya hivi karibuni, zikiwamo shutuma juu ya jinsi alivyoushughulikia mzozo wa wahamiaji.

Suala hilo limesababisha kushuka kwa umashuhuri wake na kuja juu kwa siasa za sera kali za mrengo wa kulia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ujerumani (DPA), wakati akitangaza ugombea wake kwa wanachama waandamizi wa CDU, pia alisema atawania kukiongoza tena chama hicho cha sera za mrengo wa wastani wa kulia.

Kwa mujibu wa kura za maoni zilizochapishwa katika gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag, asilimia 55 ya Wajerumani wanataka Merkel aendelee kuongoza kwa miaka mingine minne wakati asilimia 39 ilipinga.

Merkel ameliongoza taifa hilo lenye nguvu kubwa kiuchumi barani Ulaya kupitia msukosuko wa kifedha na mzozo wa madeni wa nchi zinazotumia sarafu ya euro.

Kwa sababu hizo na nyingine, amejipatia heshima ya kimataifa huku Rais Barack Obama wa Marekani alipokuwa ziarani nchini hapa akimwelezea ni ‘mshirika wa kupigiwa mfano.’

Kutokana na ushindi wa Trump nchini Marekani, kuongezeka kuungwa mkono kwa vyama vya sera kali za mrengo wa kulia barani Ulaya, baadhi ya wachambuzi wanamwona Merkel kuwa ngome ya maadili ya kiliberali.

Hata hivyo, uamuzi wake wa mwaka jana kuruhusu takriban wahamiaji 900,000 wengi wao kutoka maeneo ya vita Mashariki ya Kati, umewakasirisha wapigakura wengi nyumbani na kuathiri umaarufu wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles