24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Yaliyojiri tuzo za American Music Awards (AMA)

BADI MCHOMOLO NA MITANDAO


rihanna

MTANZANIA linakuletea mambo mbalimbali yaliyotokea katika utoaji wa tuzo za American Music Awards (AMA) zilizofanyika usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa Microsoft Theater, uliopo Los Angeles, Marekani kama ifuatavyo;

Wavunja rekodi

Wakali wa muziki wa Pop kutoka Canada, Aubrey Drake na Justine Bieber wamevunja rekodi ya aliyekuwa mfalme wa muziki wa pop duniani, Michael Jackson, baada ya kunyakua tuzo nne kila mmoja katika tuzo hizo.

Drake amenyakua tuzo ya msanii bora wa mwaka, msanii wa hip hop anayependwa, albamu ya hip hop inayopendwa ‘Views’, wimbo wa hip hop unaopendwa ‘Hotline bling’.

Beiber amenyakua tuzo ya video bora ya mwaka ‘Sorry’, msanii wa kiume wa muziki wa Pop anayependwa, albamu inayopendwa zaidi ya Pop ‘Purpose’ na wimbo unaopendwa wa Pop ‘Love Yourself’.

Licha ya kunyakua tuzo hizo nne, jina la Drake kwa mara ya kwanza lilikuwa katika vipengele 13, lakini akanyakua tuzo nne na Bieber naye alikuwa akiwania tuzo sita akanyakua nne.

Tangu tuzo hizo zilipoanza mwaka 1972, Michael Jackson ndiye msanii pekee aliyeweka historia ya jina lake kuwa katika vipengele 11 mwaka 1984 hadi Drake alipoivunja rekodi hiyo mwaka huu kwa kuwa katika vipengele 13.

Hata hivyo, Drake aliwataka mashabiki wake kutumia jina lake vizuri, huku akijinadi kuwapoteza kimuziki wasanii wenye majina makubwa zaidi yake.

Rihanna

Mkali wa muziki wa RnB, Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ alifuata kwa idadi kubwa ya tuzo baada ya kujinyakulia tuzo tatu, huku Twenty One Pilots nao wakinyakua tuzo mbili.

Rihanna amenyakua tuzo ya wimbo bora unaopendwa wa RnB ‘Work’, albamu ya RnB inayopendwa ‘Anti’ na msanii wa kike wa RnB anayependwa.

Mshiriki X-Factor

Nyota wa muziki kutoka nchini Uingereza, Zayn Malik, aliwahi kuwa mshiriki bora wa shindano la muziki la X-Factor 2010, licha ya kunyakua tuzo la msanii bora wa mwaka chipukizi, alitoa kituko kwa kudai kwamba hatawashukuru waliokuwa mashabiki wake tangu alipoanza muziki, bali anawashukuru mashabiki wake wapya waliomsaidia kupata tuzo aliyoipata.

“Siwezi kuwashukuru wote waliokuwa na mimi tangu nilipoanza muziki, inatosha kwa kile walichokifanya, huu ni wakati wa kuwashukuru wengine wapya,” alieleza Malik.

Tuzo mbalimbali

Wasanii wengine waliopata tuzo moja ni pamoja na Ariana Grande, Beyonce, Chris Brown, Selena Gomez, Fifth Harmony, Blake Shelton, Florida Georgia Line, Carrie Underwood na Tim McGraw.

Wengine ni Adele, Enrique Iglesias, Hillsong United, The Chainsmokers, Purple Rain na Adele.

Walionogesha

Wasanii wengine ambao waliwagusa mashabiki kutokana na shoo kali ni pamoja na John Legend kutokana na wimbo wake wa ‘Love Me Now’, wengine ni Ariana Grande na Nicki Minaj, ambao walipiga shoo ya kuvutia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles