Mbunge Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) anashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa akiwa jukwaani katika mkutano wa hadhara, jimboni kwake.
Msigwa amekamatwa leo Septemba 24, saa 11.30 jioni wakati mbunge huyo akiwa anahutubia wananchi wa Kata ya Mlandege jimboni humo, ghafla jukwaa hilo lilizungukwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), na kumtaka kushuka jukwaani ambapo alitii na moja kwa moja walimpeleka Kituo cha Polisi cha Iringa Mjini ambako anashikiliwa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amethibitisha kukamatwa kwa Msigwa ambapo amesema taarifa zaidi za sababu ya kukamatwa kwake itatolewa baadaye.