24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

MCHUNGAJI AMTABIRIA USHINDI UHURU KENYATTA

NA PATRICIA KIMELEMETA

MCHUNGAJI wa Kanisa la Mitume na Manabii, Daudi Mashimo, ametabiri kuwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ana nafasi kubwa ya kushinda kwenye uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26, mwaka huu.

Kenyatta ni mgombea anayetokea kwenye vyama vilivyounda Jubilee wakati mpinzani wake anatokea kwenye vyama vya muungano wa Nasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mashimo alisema awali alitabiri kuwa uchaguzi huo utafanyika na Kenyatta kupata ushindi lakini utavurugika baada ya mpinzani wake ambaye ni Raila Odinga kupinga matokeo mahakamani.

Alisema kutokana na hali hiyo, licha ya kutokea kwa vurugu za hapa na pale, lakini Kenyatta anashinda kwenye uchaguzi huo wa marudio hali ambayo pia itamfanya Odinga kutoamini.

“Nimepata maono kuwa uchaguzi wa marudio unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini Kenya, Uhuru Kenyatta, atashinda kama alivyoshinda awali kwa sababu nimepata maono kuhusiana na nchi hiyo,” alisema Mashimo.

Aliongeza, hata hivyo katika uchaguzi huo, Odinga hatakubali matokeo tena na kusababisha kujitokeza kwa vurugu za hapa na pale.

Alisema katika uchaguzi huo, Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo (IEBC), itasimamia uchaguzi huo kwa haki bila ya kupendelea upande wowote, lakini kitakachomfanya Odinga kupinga ni pamoja na kutokuwa na imani na tume hiyo tangu awali, hali iliyosababisha kupinga matokeo ya mwanzo.

Mchungaji Mashimo aliwashauri wananchi wa Kenya kuepuka vurugu zitakazosababishwa na wanasiasa hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya wananchi wasio na hatia.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles